Posts

Showing posts from January, 2025

DEO MECK Apongeza CCM kwa Kumchagua Stephen Wasira Kuwa Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara

Image
Pichani ni Mdau wa Maendeleo na kada wa Ccm Ndg DEO MECK Mwanachama na mdau wa maendeleo, Deo Meck, amepongeza Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwa kumchagua Stephen Wasira kuwa Makamu Mwenyekiti wa CCM Tanzania Bara. Meck amesema kuwa uteuzi huo ni hatua sahihi kwa chama, kwani Wasira ni kiongozi mwenye uzoefu mkubwa, anayejua misingi ya chama, na mwenye maono thabiti kwa maendeleo ya taifa. Akizungumza na waandishi wa habari, Meck alisema kuwa Wasira ana rekodi nzuri ya uongozi, akibainisha kuwa amekuwa mstari wa mbele katika kuhimiza nidhamu, umoja, na mshikamano ndani ya chama. Alisisitiza kuwa uamuzi wa CCM kumchagua Wasira unaonyesha kuwa chama kinatambua mchango wa viongozi wenye uadilifu na walio tayari kuendeleza misingi ya chama kwa manufaa ya Watanzania wote. "Wasira ni mtu makini, ana uzoefu wa muda mrefu ndani ya chama na serikali. Amejitoa kwa hali na mali kuhakikisha kuwa misingi ya chama inaheshimiwa na maendeleo ya wananchi yanapewa kipaumbele. Uteuzi wake ni wa busara, ...

Mwenyekiti wa Mtaa wa Sabasaba, Mji wa Tarime, ameonyesha hatua kubwa ya kuunga mkono elimu kwa watoto wa familia maskini

Image
pichani ni wanafunzi pamoja na mwenyekiti wa mtaa wa sabasaba Mhe Sabato amos Mwenyekiti wa Mtaa wa Sabasaba, Mji wa Tarime, ameonyesha hatua kubwa ya kuunga mkono elimu kwa watoto wa familia maskini katika mtaa huo kwa kuwapatia uniform na madaftari watoto 18 ambao walikuwa wamekosa fursa ya kujiunga na shule kwa sababu ya ukosefu wa vifaa vya shule muhimu. Hatua hii imekuja baada ya kubaini kwamba watoto hao walikosa nafasi ya kujifunza kutokana na changamoto ya kifedha, na hivyo, wenyekiti aliona ni muhimu kuhakikisha wanapata vifaa hivyo ili waweze kurudi darasani. Akizungumza wakati wa kutoa msaada huo, mwenyekiti wa mtaa alisisitiza umuhimu wa elimu kwa watoto kama nguzo kuu ya maendeleo katika jamii. Alieleza kuwa msaada huo unalenga kuwapa watoto hawa fursa ya kupata elimu bora, ambayo itawawezesha kujijenga kimaisha na kuchangia katika maendeleo ya jamii yao. "Tunapojitahidi kuleta maendeleo, hatuwezi kufanikisha bila kuwajali watoto wetu. Hawa ni viongozi wa kesho, na t...

MKUU WA DAWATI LA JINSIA NA WATOTO MKOA WA LINDI ASAIDIA WATOTO WANAOTOKA KATIKA MAZINGIRA MAGUMU KWA KUWAPATIA SALE ZA SHULE ILI WAWEZE KUENDELEA NA MASOMO YAO

Image
  Mkuu wa kitengo cha Dawati la Jinsia na watoto Mkoa wa Lindi Inspecta Msaidizi wa Jeshi la Polisi JOYCE KITESHO ameweza kuwakabidhi sale za shule wanafunzi 15 wanaotoka katika familia zenye mazingira magumu katika manispaa ya Lindi Mkoani Lindi . Mnamo mwezi Novemba mwaka uliopita 2024 Joyce Kitesho aliweza kufanya ziara na kutembelea shule ya msingi Ruaha iliyopo manispaa ya Lindi Mkoani Lindi ambapo aliweza kubaini changamoto kwa wanafunzi hao ambao wwngi wao wanatoka katika familia zisizojiweza ambapo aliwakuta wanafunzi hao wakiwa wamevaa sale za shule ( Uniform) zilizochakaa na kuchanika huku wwngine wakiwa hawana kabisa badala yake wamevaa nguo za nyumbani . Hali hiyo ikamgusa Kiongozi huyo ambapo hii leo amefika shuleni hapo katika mwaka huu wa masomo 2025 mwezi huu January ambapo ameweza kukabidhi sale za shule kwa watoto 15 katika shule ya msingu Ruaha iliyopo manispaa ya Lindi Mkoani humo.  Inspecta msaidizi wa Jeshi la polisi Joyce Kitesho ambaye ni Mkuu wa Dawa...