MKUU WA DAWATI LA JINSIA NA WATOTO MKOA WA LINDI ASAIDIA WATOTO WANAOTOKA KATIKA MAZINGIRA MAGUMU KWA KUWAPATIA SALE ZA SHULE ILI WAWEZE KUENDELEA NA MASOMO YAO
Mkuu wa kitengo cha Dawati la Jinsia na watoto Mkoa wa Lindi Inspecta Msaidizi wa Jeshi la Polisi JOYCE KITESHO ameweza kuwakabidhi sale za shule wanafunzi 15 wanaotoka katika familia zenye mazingira magumu katika manispaa ya Lindi Mkoani Lindi .
Mnamo mwezi Novemba mwaka uliopita 2024 Joyce Kitesho aliweza kufanya ziara na kutembelea shule ya msingi Ruaha iliyopo manispaa ya Lindi Mkoani Lindi ambapo aliweza kubaini changamoto kwa wanafunzi hao ambao wwngi wao wanatoka katika familia zisizojiweza ambapo aliwakuta wanafunzi hao wakiwa wamevaa sale za shule ( Uniform) zilizochakaa na kuchanika huku wwngine wakiwa hawana kabisa badala yake wamevaa nguo za nyumbani .
Hali hiyo ikamgusa Kiongozi huyo ambapo hii leo amefika shuleni hapo katika mwaka huu wa masomo 2025 mwezi huu January ambapo ameweza kukabidhi sale za shule kwa watoto 15 katika shule ya msingu Ruaha iliyopo manispaa ya Lindi Mkoani humo.
Inspecta msaidizi wa Jeshi la polisi Joyce Kitesho ambaye ni Mkuu wa Dawati la Jinsia na watoto Mkoa wa Lindi amesisitiza wazazi pamoja na walezi kuhakikisha wanawapa haki ya kupata Elimu kama haki ya msingi ya mtoto ambaye anastahili kisheria .








Comments
Post a Comment