Posts

Showing posts from 2026

MBUNGE ESTHER BULAYA ASHIRIKI HAFLA YA UGAWAJI WA SARUJI MKOA WA MARA

Image
Pichani ni Mbunge wa Jimbo la Bunda Mjini akipokea Saruji Toka Nyansaho foundation Mbunge wa Jimbo la Bunda Mjini, Esther Bulaya, tarehe 22 Machi 2026 alishiriki katika hafla ya ugawaji wa mifuko ya saruji iliyofanyika katika ukumbi wa Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Mara uliopo Musoma. Hafla hiyo ilihudhuriwa na viongozi mbalimbali wa kisiasa kutoka majimbo ya Mkoa wa Mara pamoja na wananchi waliokusanyika kushuhudia tukio hilo muhimu la maendeleo. Hafla hiyo iliandaliwa na Nyansaho Foundation chini ya uongozi wa Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Rhimo Nyansaho, ambaye pia alikuwa mgeni rasmi katika tukio hilo. Taasisi hiyo imekuwa ikifanya shughuli mbalimbali za kijamii zenye lengo la kusaidia jamii katika maeneo tofauti ya maendeleo. Lengo kuu la hafla hiyo lilikuwa ni kugawa mifuko ya saruji kwa majimbo yote 11 ya Mkoa wa Mara. Msaada huo umetolewa kwa lengo la kusaidia utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo katika jamii, ikiwemo ujenzi wa miundombinu muhimu kama shule...

BULAYA AUNGANA NA VIJANA BODA BODA, ATOA MSAADA NA KUHIMIZA AMANI

Image
                            PICHANI NI  MHE. ESTHER BULAYA AKIWA NA MAAFISA USAFILISHAJI WA BUNDA STOO Na mwandishi wetu Bunda mjini  Mbunge wa Jimbo la Bunda Mjini, Esther Bulaya, ametembelea vijana wa kituo cha bodaboda Bunda Stoo na kushiriki nao mazungumzo yenye kujenga mshikamano na maendeleo ya vijana. Katika ziara hiyo, Mhe. Bulaya alionyesha kuguswa na hali ya kijiwe chao na kutoa msaada wa kiasi cha shilingi 250,000 kwa ajili ya ukarabati, ili kuboresha mazingira yao na kupata kivuli bora wakati wa shughuli zao za kila siku. Bulaya akiteta na maafisa usafilishaji Aidha, alimsaidia kijana mmoja kwa kumpatia fedha za kufanya marekebisho ya pikipiki yake, akilenga kuongeza usalama barabarani na kuboresha kipato chake kupitia kazi ya usafirishaji. Mbali na misaada hiyo, Mhe. Bulaya alitoa elimu na mawaidha kwa vijana hao, akiwataka kuwa makini na watu wanaoweza kuwatumia vibaya kwa maslahi binafsi. Aliw...

Kisangwa Yapata Neema ya Maji: Esther Bulaya Ashiriki Uzinduzi wa Mradi wa Milioni 716 Bunda

Image
MBUNGE WA BUNDA MJINI MHE. ESTHER BULAYA    Wananchi wa Kata ya Mchalo, tawi la Kisangwa, Wilaya ya Bunda wamepata tumaini jipya baada ya kuzinduliwa rasmi kwa jiwe la msingi la mradi wa maji unaolenga kuondoa changamoto ya uhaba wa huduma hiyo muhimu. Mbunge wa Bunda Mjini, Esther Bulaya, leo Machi 17, 2026 alishiriki katika uzinduzi huo uliokwenda sambamba na maadhimisho ya Wiki ya Maji, tukio lililokusanya viongozi wa kisiasa, wataalamu wa sekta ya maji pamoja na wananc hi wa eneo hilo. Uzinduzi huo uliongozwa na Mkuu wa Wilaya ya Bunda, Aswege Enock Kaminyoge, aliyemwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Mara, Evans Mtambi, huku ukihudhuriwa pia na Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Bunda (BUWASA), Esther Enock Gilyoma, pamoja na viongozi mbalimbali wa idara ya maji. Akizungumza katika hafla hiyo, Bulaya alieleza kuwa mradi huo wenye thamani ya shilingi milioni 716 ni sehemu ya jitihada za Serikali kuhakikisha wananchi wanapata huduma safi na salama ya maji, huku ...

Mheshimiwa Esther N. Matiko Aanza Ziara Tarime Mjini kwa Kishindo, Aahidi Kutatua Kero za Wananchi

Image
 Mbunge wa Tarime Mjini, Esther N. Matiko, ameanza rasmi ziara yake jimboni kwa kishindo kwa kutembelea Kata ya Ketare, ambapo amekutana na wananchi, kusikiliza changamoto zao na kuahidi kuzifanyia kazi kwa haraka. Asikiliza Kero za Wananchi Ketare Katika mkutano uliofanyika Ketare, wananchi walipata nafasi ya kuwasilisha kero mbalimbali zinazowakabili, ikiwemo changamoto za miundombinu ya barabara, huduma za maji, na masuala ya maendeleo ya kijamii. Mbunge huyo alisisitiza kuwa lengo la ziara yake ni kusikiliza sauti za wananchi moja kwa moja ili kupata uhalisia wa changamoto zilizopo na kuzitafutia ufumbuzi wa kudumu. Alieleza kuwa ofisi yake itaendelea kushirikiana na viongozi wa serikali za mitaa na mamlaka husika kuhakikisha kila hoja inayowasilishwa inapewa uzito unaostahili. Serikali Yatenga Fedha kwajili ya Nyamwaga Road Akizungumzia kwa kina kero ya barabara ya Nyamwaga Road, Mbunge huyo alisema kuwa tayari Serikali imetenga kiasi cha fedha kwa ajili ya ujenzi na uboreshaj...