Posts

Showing posts from October, 2025

KWA NINI SAMIA SULUHU HASSAN ANASTAHILI KURA ZA USHINDI KWA MARA NYINGINE

Image
DR SAMIA SULUHU HASSAN Na Daniel Mussa MBC MEDIA Tanzania iko katika kipindi cha mageuzi makubwa ya maendeleo, umoja, na diplomasia chini ya uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan. Tangu aingie madarakani mwaka 2021, Mama Samia amethibitisha kwa vitendo kuwa ni kiongozi mwenye maono, busara, na moyo wa kujenga taifa linaloangalia mbele. Ni kutokana na kazi yake kubwa na dira yake thabiti, Watanzania wana kila sababu ya kumpa tena kura za ushindi ili aendelee kuiongoza nchi kwa kipindi kingine cha miaka mitano. Kwanza, Mama Samia amerejesha heshima ya Tanzania kimataifa. Kupitia diplomasia yake ya ucheshi, usikivu na utulivu, ameweka taifa katika ramani ya dunia. Leo hii Tanzania ni kivutio kwa wawekezaji, watalii, na mashirika ya kimataifa, jambo lililoongeza ajira na kipato cha taifa. Pili, ameweka msukumo mkubwa katika maendeleo ya watu. Kupitia miradi mikubwa ya elimu, afya, maji na miundombinu, Mama Samia amegusa maisha ya Watanzania moja kwa moja. Elimu bure imepanuliwa, huduma za af...

ALKOS ELUTION PLANT YAIKONGA SOYA ONE LIMITED KWA USHIRIKIANO MZURI NA JAMII

Image
PICHANI NI WAFANYAKAZI WA SOYA ONE LIMITED PAMOJA NA ALKOS ELUTION WAKIWA NA VIONGOZI WAO Na Daniel Mussa, MBC Media Online News – Tarime TARIME, Oktoba 2025 Kampuni ya Alkos Elution Plant, inayojihusisha na uchenjuaji wa madini na yenye makao yake mtaa wa Zaka Filling, Nkende  Tarime Mjini, imeipongeza kampuni ya Soya One Limited kwa kuwa mdau mkubwa wa maendeleo na mshirika wa kweli wa jamii. Akizungumza katika hafla ya kuadhimisha Wiki ya Mteja iliyofanyika katika ofisi za Alkos Elution Plant, viongozi wa kampuni hiyo walimshukuru Mkurugenzi wa Soya One Limited, Ndugu Chacha Soya, kwa kukubali mwaliko wao na kuhudhuria kama mgeni rasmi katika tukio hilo muhimu. Kwa mujibu wa viongozi wa Alkos Elution Plant, ushirikiano kati ya kampuni hizo mbili umechangia kuimarisha uhusiano kati ya sekta binafsi na jamii, sambamba na kusaidia utekelezaji wa miradi ya kijamii na maendeleo ya kiuchumi ndani ya Wilaya ya Tarime. “Tunampongeza Ndugu Chacha Soya kwa moyo wake wa uzalendo na ushirik...