MBUNGE ESTHER BULAYA ASHIRIKI HAFLA YA UGAWAJI WA SARUJI MKOA WA MARA
Pichani ni Mbunge wa Jimbo la Bunda Mjini akipokea Saruji Toka Nyansaho foundation Mbunge wa Jimbo la Bunda Mjini, Esther Bulaya, tarehe 22 Machi 2026 alishiriki katika hafla ya ugawaji wa mifuko ya saruji iliyofanyika katika ukumbi wa Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Mara uliopo Musoma. Hafla hiyo ilihudhuriwa na viongozi mbalimbali wa kisiasa kutoka majimbo ya Mkoa wa Mara pamoja na wananchi waliokusanyika kushuhudia tukio hilo muhimu la maendeleo. Hafla hiyo iliandaliwa na Nyansaho Foundation chini ya uongozi wa Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Rhimo Nyansaho, ambaye pia alikuwa mgeni rasmi katika tukio hilo. Taasisi hiyo imekuwa ikifanya shughuli mbalimbali za kijamii zenye lengo la kusaidia jamii katika maeneo tofauti ya maendeleo. Lengo kuu la hafla hiyo lilikuwa ni kugawa mifuko ya saruji kwa majimbo yote 11 ya Mkoa wa Mara. Msaada huo umetolewa kwa lengo la kusaidia utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo katika jamii, ikiwemo ujenzi wa miundombinu muhimu kama shule...