Mheshimiwa Esther N. Matiko Aanza Ziara Tarime Mjini kwa Kishindo, Aahidi Kutatua Kero za Wananchi
Mbunge wa Tarime Mjini, Esther N. Matiko, ameanza rasmi ziara yake jimboni kwa kishindo kwa kutembelea Kata ya Ketare, ambapo amekutana na wananchi, kusikiliza changamoto zao na kuahidi kuzifanyia kazi kwa haraka. Asikiliza Kero za Wananchi Ketare Katika mkutano uliofanyika Ketare, wananchi walipata nafasi ya kuwasilisha kero mbalimbali zinazowakabili, ikiwemo changamoto za miundombinu ya barabara, huduma za maji, na masuala ya maendeleo ya kijamii. Mbunge huyo alisisitiza kuwa lengo la ziara yake ni kusikiliza sauti za wananchi moja kwa moja ili kupata uhalisia wa changamoto zilizopo na kuzitafutia ufumbuzi wa kudumu. Alieleza kuwa ofisi yake itaendelea kushirikiana na viongozi wa serikali za mitaa na mamlaka husika kuhakikisha kila hoja inayowasilishwa inapewa uzito unaostahili. Serikali Yatenga Fedha kwajili ya Nyamwaga Road Akizungumzia kwa kina kero ya barabara ya Nyamwaga Road, Mbunge huyo alisema kuwa tayari Serikali imetenga kiasi cha fedha kwa ajili ya ujenzi na uboreshaj...