Posts

Showing posts from June, 2025

SOYA ONE LIMITED YAMUUNGA MKONO MHANDISI WA MADINI MKOA WA MARA, YAMPA PONGEZI KWA UTENDAJI WAKE BORA

Image
PICHANI NI MHANDISI MSUYA OFISI YA MADINI MKOA WA MARA Tarime, Juni 7, 2025 Kampuni ya Soya One Limited chini ya uongozi wa Mkurugenzi wake mahiri, Chacha Soya, imetoa pongezi za dhati kwa Mhandisi wa Madini Mkoa wa Mara, Mhandisi Amin Msuya, kwa kazi nzuri na ya mfano anayofanya katika kusimamia sekta ya madini mkoani humo. Kupitia taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa leo, Chacha Soya alisema kuwa kampuni yake, ambayo inajihusisha na shughuli za uchimbaji na usimamizi wa madini kwa kuzingatia misingi ya uwajibikaji kwa jamii, imeridhishwa na namna ambavyo ofisi ya Afisa Madini Mkazi wa Mkoa wa Mara inatekeleza majukumu yake kwa weledi, uwazi na kasi inayolenga maendeleo ya wachimbaji na ustawi wa uchumi wa mkoa. > "Kwa niaba ya Soya One Limited, napenda kumpongeza Mhandisi Amin Msuya kwa kazi nzuri anayoifanya. Ameonesha mfano wa uongozi bora kwa kushirikiana na wadau wote wa sekta ya madini bila ubaguzi, huku akihakikisha mazingira rafiki ya uwekezaji na uchimbaji yanaim...

SOYA ONE LIMITED YAIPONGEZA SERIKALI KWA KUWAWEZESHA WACHIMBAJI WADOGO NA KUIUNGA MKONO SEKTA YA MADINI

Image
PICHANI NI MKURUGENZI WA SOYA ONE LIMITED NDG CHACHA SOYA MUSOMA, JUNI 7, 2025 Kampuni ya Soya One Limited imetoa pongezi za dhati kwa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa hatua madhubuti inazochukua katika kuwawezesha na kuwashika mkono wachimbaji wadogo wadogo wa madini nchini, hususan katika mkoa wa Mara. Akizungumza mara baada ya kukamilika kwa kongamano kubwa la wachimbaji wa madini wa Mkoa wa Mara lililofanyika tarehe 6 Juni 2025 katika viwanja vya Mkendo, Musoma Mjini, Mkurugenzi wa Soya One Limited, Ndugu Chacha Soya, amesema kuwa mafanikio ya sekta ya madini yanaakisi juhudi za serikali ya awamu ya sita katika kuhakikisha wachimbaji wadogo wanapewa mazingira bora ya kufanya kazi kwa tija na usalama. "Natoa shukrani za dhati kwa Serikali kwa kuendelea kutambua mchango wa wachimbaji wadogo, lakini zaidi kwa hatua ya kuwajengea uwezo na kuwawekea mazingira rafiki ya kuchangia pato la taifa," alisema Ndugu Chacha Soya. "Sisi kama Soya One Limited, tunaion...

GWAJIMA AACHE KUCHEZEA AMANI YA TAIFA, NA MHE. RAIS SAMIA AANGALIE JICHO LA CHINI YA KIVULI HIKI

Image
PICHANI NI MWANAHABARI DANIEL MUSSA Na: Daniel Mussa Mwanahabari, Mtanzania Mzalendo, Tarime Kuna wakati wa kukaa kimya. Na kuna wakati wa kusimama na kusema kwa nguvu zote. Sasa ni ule wakati. Kwa siku kadhaa sasa, taifa letu limetikiswa na kauli za Askofu Josephat Gwajima Mbunge wa Kawe, ambaye badala ya kutenda kazi za uongozi na uwakilishi, amegeuza jukwaa lake kuwa kiwanda cha tuhuma, vitisho, na propaganda chafu. Amediriki kutumia jina la hayati Dkt. John Pombe Magufuli akijivika mavazi ya mashujaa, ilhali kwa ndani akipanda mbegu za uchochezi. Kauli yake ya “nileteeni Gwajima” ambayo aliwahi kusemewa na Magufuli, sasa anaitumia kama kibali cha kuasi nidhamu ya chama, kupinga serikali, na kudhoofisha jitihada za Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan katika kulijenga taifa la maridhiano, mageuzi ya kiuchumi, na diplomasia ya matumaini. Pichani ni Mheshimiwa Joseph Gwajima Hivi tunamwambiaje Rais Samia anayepambana kila siku kusafisha nchi na kuijenga upya, kuwa kuna watu wanaomchimba kisi...

SOYA ONE LIMITED YAKONGA NYOYO ZA WAUGUZI TARIME MJINI – YACHANGIA MAMILIONI KWENYE HARAMBEE YA UNUNUZI WA GARI LA WAFANYAKAZI WA AFYA

Image
  Pichani ni Mkurugenzi wa kampuni ya Soya One Limited  Na Daniel Mussa, Tarime Katika kuendeleza moyo wa uwajibikaji kwa jamii, kampuni ya SOYA ONE LIMITED, inayojishughulisha na uchimbaji wa madini na yenye makao yake katika Kata ya Kenyamanyori, wilayani Tarime, imetoa mchango mkubwa wa fedha katika harambee ya kuchangia ununuzi wa gari kwa ajili ya wafanyakazi wa afya wa Halmashauri ya Mji Tarime. Shughuli hiyo ilifanyika katika ukumbi wa BlueSky, ambapo ilihudhuriwa na mamia ya watumishi wa sekta ya afya, viongozi wa serikali, na wadau wa maendeleo. Mkurugenzi wa SOYA ONE LIMITED, Bw. Chacha Soya, alikuwa mgeni rasmi na alikabidhi mchango wa mamilioni ya shilingi kusaidia kutimiza azma ya ununuzi wa gari aina ya Coster, litakalosaidia katika usafiri wa pamoja wa wafanyakazi wa afya kwa shughuli mbalimbali. "Tumeguswa na dhamira ya watumishi wetu wa afya kutafuta suluhisho la changamoto zao kupitia harambee. Kama SOYA ONE LIMITED, hatukusita kushiriki kwa moyo mmoja kwa sa...