MBUNGE VITI MAALUM GHATI CHOMETE NA MBARAZA MARIAM SAGINI WAAHIDI KUONGEZA WANAFUNZI CHUO CHA LAKE VICTORIA DISABILITY VOCATIONAL TRAINING CENTRE
Mbunge Viti Maalumu Mkoa wa Mara Mhe. Ghati Chomete ameahidi kushirikiana na Mjumbe wa Baraza Kuu UWT Taifa Ndg. Mariam Sagini kuhamasisha na kukitangaza Chuo cha Lake Victoria Disability Vocational Training Centre ili wanafunzi waongezeke kutokana na uwezo wake wa kubeba wanafunzi zaidi 600 ila mpaka sasa kina wanafunzi 65. Akizungumza wakati alipomwakilisha Mgeni Rasmi Mjumbe wa Baraza Kuu UWT Taifa Ndg. Mariam Sagini katika mahafali ya nane yaliyofanyika chuoni hapo Novemba 22, 2024 katika Kijiji cha Nyabange, Kata ya Nyankanga, Wilaya ya Butiama Mhe. Chomete amesema chuo hicho kina mchango mkubwa katika kuwapa vijana wenye ulemavu na wasio na ulemavu fursa ya kujifunza na kujiendeleza. "Habari njema ni kwamba chuo hiki pamoja na kutoa huduma ya elimu ya ufundi nimeambiwa mnatoa huduma ya utengamao kwa watu wenye ulemavu kama mazoezi tiba, kazi tiba, utengenezaji wa viungo bandia, vifaa saidizi kama baiskeli za watu wenye ulemavu, magongo ya kutembelea, viti vya kona nk. Hii in...