Na Happiness Shayo -Ikungi Waziri wa Maliasili na Utalii,Mhe. Balozi, Dkt. Pindi Chana (Mb) ameelekeza timu ya Askari Uhifadhi 18 kuweka kambi katika Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi Mkoani Singida kwa lengo la kukabiliana na tembo wanaovambia makazi ya watu. Hatua hiyo inafuatiwa na tukio la hivi karibuni la tembo kuwepo katika eneo hilo na kusababisha taharuki kwa wananchi. Akizungumza na wananchi katika Mkutano wa hadhara leo Oktoba 28,2024 kwenye Kijiji cha Mkiwa Wilaya ya Ikungi, Mkoani Singida Mhe. Chana amesema nia ya Serikali ni kuhakikisha changamoto ya wanyamapori wakali na waharibifu hususan tembo inapungua au kumalizika kabisa. "Tunakwenda kuongeza askari watakaotusaidia kuhakikisha tembo wanarudi katika maeneo yao ya hifadhi sambamba na kuongeza mabomu baridi kufukuza tembo" Mhe. Chana amesisitiza. Aidha, amesema Wizara ya Maliasili na Utalii kwa kushirikiana na Serikali za Vijiji,Wilaya na Mkoa itafanya zoezi la kutambua na kuweka alama katika maeneo ya Korido...