Posts

Showing posts from December, 2025

MKURUGENZI WA SOYA ONE LIMITED AWASISITIZA WAUMINI WA EAGT RONSOTI TARIME MJINI KUILINDA AMANI; AFANIKISHA UPATIKANAJI WA MCHANGO WA MILIONI 12, ACHANGIA MILIONI 8 NA ASINDIKIZWA KWA MILIONI 5

Image
MKURUGENZI WA SOYA ONE LIMITED  (CHACHA GESORA)  Tarime Mjini, Tanzania – Mkurugenzi wa Soya One Limited, Chacha Soya, ameendelea kuonyesha moyo wa kujitoa kwa jamii baada ya kufanikisha upatikanaji wa mchango wa jumla ya shilingi milioni 12, ambapo mwenyewe alichangia milioni 8, na waumini pamoja na wageni wengine wakasindikiza kwa milioni 5. Mkurugenzi huyo alialikwa rasmi kama mgeni maalum katika ibada ya Jumapili iliyofanyika katika Kanisa la EAGT Ronsoti, ibada iliyojaa uwepo wa Mungu na iliyoongozwa na Mchungaji Maswi. Katika hotuba yake yenye kugusa mioyo, Mkurugenzi Soya alisisitiza umuhimu wa kulinda amani ya nchi akisema: “Amani yetu ni nguzo ya maendeleo. Tanzania imebarikiwa na Mungu kwa utulivu wake. Tuilinde, tuiombee, na tuishi kama watu wanaothamini urithi huu adhimu.” Alisisitiza kuwa amani ndiyo msingi wa ibada, biashara, uchumi na ustawi wa familia, hivyo kila Mwanatarime na Mtanzania kwa ujumla ana wajibu wa kuwa mlinzi wa amani. Katika kuendelea kusapoti k...