Posts

Showing posts from July, 2025

MKUU WA WILAYA YA TARIME AKABIDHI MIZINGA KWA WAZEE WA KOO 12 WAZEE WAMSHUKURU NA KUTOA PONGEZI KWA SOYA ONE NA WADAU WENGINE

Image
  Tarime, Julai 28, 2025 Mkuu wa Wilaya ya Tarime, Meja Edward Gowele, ameendesha tukio maalum la kukabidhi mizinga ya nyuki kwa wazee wa koo zote kumi na mbili za Tarime Mjini na Vijijini, ikiwa ni hatua ya kuwaheshimu, kuwawezesha kiuchumi, na kutambua mchango wao mkubwa katika kulinda amani na utulivu wa jamii. Akizungumza katika hafla hiyo, Meja Gowele alisema kuwa wazee ni nguzo kuu ya hekima, mshikamano na maadili katika jamii, hivyo ni wajibu wa serikali na jamii kwa ujumla kuendelea kuwathamini na kuwawezesha ili waweze kushiriki kikamilifu kwenye maendeleo. “Leo tunawakabidhi mizinga hii ya nyuki si tu kama njia ya kuwawezesha kiuchumi, bali kama alama ya heshima na shukrani kwa nafasi yenu muhimu katika jamii. Mmetufundisha kuwa amani huanza nyumbani, na nyinyi mmekuwa walinzi wakuu wa hilo,” alisema Meja Gowele. Katika hatua ya kuonyesha mshikamano wa pamoja, Mkuu huyo wa Wilaya aliwashukuru kwa dhati wadau wote walioguswa na kutoa mchango wao kufanikisha zoezi hilo. Wad...