Posts

Showing posts from 2025

MKURUGENZI WA SOYA ONE LIMITED AWASISITIZA WAUMINI WA EAGT RONSOTI TARIME MJINI KUILINDA AMANI; AFANIKISHA UPATIKANAJI WA MCHANGO WA MILIONI 12, ACHANGIA MILIONI 8 NA ASINDIKIZWA KWA MILIONI 5

Image
MKURUGENZI WA SOYA ONE LIMITED  (CHACHA GESORA)  Tarime Mjini, Tanzania – Mkurugenzi wa Soya One Limited, Chacha Soya, ameendelea kuonyesha moyo wa kujitoa kwa jamii baada ya kufanikisha upatikanaji wa mchango wa jumla ya shilingi milioni 12, ambapo mwenyewe alichangia milioni 8, na waumini pamoja na wageni wengine wakasindikiza kwa milioni 5. Mkurugenzi huyo alialikwa rasmi kama mgeni maalum katika ibada ya Jumapili iliyofanyika katika Kanisa la EAGT Ronsoti, ibada iliyojaa uwepo wa Mungu na iliyoongozwa na Mchungaji Maswi. Katika hotuba yake yenye kugusa mioyo, Mkurugenzi Soya alisisitiza umuhimu wa kulinda amani ya nchi akisema: “Amani yetu ni nguzo ya maendeleo. Tanzania imebarikiwa na Mungu kwa utulivu wake. Tuilinde, tuiombee, na tuishi kama watu wanaothamini urithi huu adhimu.” Alisisitiza kuwa amani ndiyo msingi wa ibada, biashara, uchumi na ustawi wa familia, hivyo kila Mwanatarime na Mtanzania kwa ujumla ana wajibu wa kuwa mlinzi wa amani. Katika kuendelea kusapoti k...

KWA NINI SAMIA SULUHU HASSAN ANASTAHILI KURA ZA USHINDI KWA MARA NYINGINE

Image
DR SAMIA SULUHU HASSAN Na Daniel Mussa MBC MEDIA Tanzania iko katika kipindi cha mageuzi makubwa ya maendeleo, umoja, na diplomasia chini ya uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan. Tangu aingie madarakani mwaka 2021, Mama Samia amethibitisha kwa vitendo kuwa ni kiongozi mwenye maono, busara, na moyo wa kujenga taifa linaloangalia mbele. Ni kutokana na kazi yake kubwa na dira yake thabiti, Watanzania wana kila sababu ya kumpa tena kura za ushindi ili aendelee kuiongoza nchi kwa kipindi kingine cha miaka mitano. Kwanza, Mama Samia amerejesha heshima ya Tanzania kimataifa. Kupitia diplomasia yake ya ucheshi, usikivu na utulivu, ameweka taifa katika ramani ya dunia. Leo hii Tanzania ni kivutio kwa wawekezaji, watalii, na mashirika ya kimataifa, jambo lililoongeza ajira na kipato cha taifa. Pili, ameweka msukumo mkubwa katika maendeleo ya watu. Kupitia miradi mikubwa ya elimu, afya, maji na miundombinu, Mama Samia amegusa maisha ya Watanzania moja kwa moja. Elimu bure imepanuliwa, huduma za af...

ALKOS ELUTION PLANT YAIKONGA SOYA ONE LIMITED KWA USHIRIKIANO MZURI NA JAMII

Image
PICHANI NI WAFANYAKAZI WA SOYA ONE LIMITED PAMOJA NA ALKOS ELUTION WAKIWA NA VIONGOZI WAO Na Daniel Mussa, MBC Media Online News – Tarime TARIME, Oktoba 2025 Kampuni ya Alkos Elution Plant, inayojihusisha na uchenjuaji wa madini na yenye makao yake mtaa wa Zaka Filling, Nkende  Tarime Mjini, imeipongeza kampuni ya Soya One Limited kwa kuwa mdau mkubwa wa maendeleo na mshirika wa kweli wa jamii. Akizungumza katika hafla ya kuadhimisha Wiki ya Mteja iliyofanyika katika ofisi za Alkos Elution Plant, viongozi wa kampuni hiyo walimshukuru Mkurugenzi wa Soya One Limited, Ndugu Chacha Soya, kwa kukubali mwaliko wao na kuhudhuria kama mgeni rasmi katika tukio hilo muhimu. Kwa mujibu wa viongozi wa Alkos Elution Plant, ushirikiano kati ya kampuni hizo mbili umechangia kuimarisha uhusiano kati ya sekta binafsi na jamii, sambamba na kusaidia utekelezaji wa miradi ya kijamii na maendeleo ya kiuchumi ndani ya Wilaya ya Tarime. “Tunampongeza Ndugu Chacha Soya kwa moyo wake wa uzalendo na ushirik...

MKUU WA WILAYA YA TARIME AKABIDHI MIZINGA KWA WAZEE WA KOO 12 WAZEE WAMSHUKURU NA KUTOA PONGEZI KWA SOYA ONE NA WADAU WENGINE

Image
  Tarime, Julai 28, 2025 Mkuu wa Wilaya ya Tarime, Meja Edward Gowele, ameendesha tukio maalum la kukabidhi mizinga ya nyuki kwa wazee wa koo zote kumi na mbili za Tarime Mjini na Vijijini, ikiwa ni hatua ya kuwaheshimu, kuwawezesha kiuchumi, na kutambua mchango wao mkubwa katika kulinda amani na utulivu wa jamii. Akizungumza katika hafla hiyo, Meja Gowele alisema kuwa wazee ni nguzo kuu ya hekima, mshikamano na maadili katika jamii, hivyo ni wajibu wa serikali na jamii kwa ujumla kuendelea kuwathamini na kuwawezesha ili waweze kushiriki kikamilifu kwenye maendeleo. “Leo tunawakabidhi mizinga hii ya nyuki si tu kama njia ya kuwawezesha kiuchumi, bali kama alama ya heshima na shukrani kwa nafasi yenu muhimu katika jamii. Mmetufundisha kuwa amani huanza nyumbani, na nyinyi mmekuwa walinzi wakuu wa hilo,” alisema Meja Gowele. Katika hatua ya kuonyesha mshikamano wa pamoja, Mkuu huyo wa Wilaya aliwashukuru kwa dhati wadau wote walioguswa na kutoa mchango wao kufanikisha zoezi hilo. Wad...

SOYA ONE LIMITED YAMUUNGA MKONO MHANDISI WA MADINI MKOA WA MARA, YAMPA PONGEZI KWA UTENDAJI WAKE BORA

Image
PICHANI NI MHANDISI MSUYA OFISI YA MADINI MKOA WA MARA Tarime, Juni 7, 2025 Kampuni ya Soya One Limited chini ya uongozi wa Mkurugenzi wake mahiri, Chacha Soya, imetoa pongezi za dhati kwa Mhandisi wa Madini Mkoa wa Mara, Mhandisi Amin Msuya, kwa kazi nzuri na ya mfano anayofanya katika kusimamia sekta ya madini mkoani humo. Kupitia taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa leo, Chacha Soya alisema kuwa kampuni yake, ambayo inajihusisha na shughuli za uchimbaji na usimamizi wa madini kwa kuzingatia misingi ya uwajibikaji kwa jamii, imeridhishwa na namna ambavyo ofisi ya Afisa Madini Mkazi wa Mkoa wa Mara inatekeleza majukumu yake kwa weledi, uwazi na kasi inayolenga maendeleo ya wachimbaji na ustawi wa uchumi wa mkoa. > "Kwa niaba ya Soya One Limited, napenda kumpongeza Mhandisi Amin Msuya kwa kazi nzuri anayoifanya. Ameonesha mfano wa uongozi bora kwa kushirikiana na wadau wote wa sekta ya madini bila ubaguzi, huku akihakikisha mazingira rafiki ya uwekezaji na uchimbaji yanaim...

SOYA ONE LIMITED YAIPONGEZA SERIKALI KWA KUWAWEZESHA WACHIMBAJI WADOGO NA KUIUNGA MKONO SEKTA YA MADINI

Image
PICHANI NI MKURUGENZI WA SOYA ONE LIMITED NDG CHACHA SOYA MUSOMA, JUNI 7, 2025 Kampuni ya Soya One Limited imetoa pongezi za dhati kwa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa hatua madhubuti inazochukua katika kuwawezesha na kuwashika mkono wachimbaji wadogo wadogo wa madini nchini, hususan katika mkoa wa Mara. Akizungumza mara baada ya kukamilika kwa kongamano kubwa la wachimbaji wa madini wa Mkoa wa Mara lililofanyika tarehe 6 Juni 2025 katika viwanja vya Mkendo, Musoma Mjini, Mkurugenzi wa Soya One Limited, Ndugu Chacha Soya, amesema kuwa mafanikio ya sekta ya madini yanaakisi juhudi za serikali ya awamu ya sita katika kuhakikisha wachimbaji wadogo wanapewa mazingira bora ya kufanya kazi kwa tija na usalama. "Natoa shukrani za dhati kwa Serikali kwa kuendelea kutambua mchango wa wachimbaji wadogo, lakini zaidi kwa hatua ya kuwajengea uwezo na kuwawekea mazingira rafiki ya kuchangia pato la taifa," alisema Ndugu Chacha Soya. "Sisi kama Soya One Limited, tunaion...

GWAJIMA AACHE KUCHEZEA AMANI YA TAIFA, NA MHE. RAIS SAMIA AANGALIE JICHO LA CHINI YA KIVULI HIKI

Image
PICHANI NI MWANAHABARI DANIEL MUSSA Na: Daniel Mussa Mwanahabari, Mtanzania Mzalendo, Tarime Kuna wakati wa kukaa kimya. Na kuna wakati wa kusimama na kusema kwa nguvu zote. Sasa ni ule wakati. Kwa siku kadhaa sasa, taifa letu limetikiswa na kauli za Askofu Josephat Gwajima Mbunge wa Kawe, ambaye badala ya kutenda kazi za uongozi na uwakilishi, amegeuza jukwaa lake kuwa kiwanda cha tuhuma, vitisho, na propaganda chafu. Amediriki kutumia jina la hayati Dkt. John Pombe Magufuli akijivika mavazi ya mashujaa, ilhali kwa ndani akipanda mbegu za uchochezi. Kauli yake ya “nileteeni Gwajima” ambayo aliwahi kusemewa na Magufuli, sasa anaitumia kama kibali cha kuasi nidhamu ya chama, kupinga serikali, na kudhoofisha jitihada za Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan katika kulijenga taifa la maridhiano, mageuzi ya kiuchumi, na diplomasia ya matumaini. Pichani ni Mheshimiwa Joseph Gwajima Hivi tunamwambiaje Rais Samia anayepambana kila siku kusafisha nchi na kuijenga upya, kuwa kuna watu wanaomchimba kisi...

SOYA ONE LIMITED YAKONGA NYOYO ZA WAUGUZI TARIME MJINI – YACHANGIA MAMILIONI KWENYE HARAMBEE YA UNUNUZI WA GARI LA WAFANYAKAZI WA AFYA

Image
  Pichani ni Mkurugenzi wa kampuni ya Soya One Limited  Na Daniel Mussa, Tarime Katika kuendeleza moyo wa uwajibikaji kwa jamii, kampuni ya SOYA ONE LIMITED, inayojishughulisha na uchimbaji wa madini na yenye makao yake katika Kata ya Kenyamanyori, wilayani Tarime, imetoa mchango mkubwa wa fedha katika harambee ya kuchangia ununuzi wa gari kwa ajili ya wafanyakazi wa afya wa Halmashauri ya Mji Tarime. Shughuli hiyo ilifanyika katika ukumbi wa BlueSky, ambapo ilihudhuriwa na mamia ya watumishi wa sekta ya afya, viongozi wa serikali, na wadau wa maendeleo. Mkurugenzi wa SOYA ONE LIMITED, Bw. Chacha Soya, alikuwa mgeni rasmi na alikabidhi mchango wa mamilioni ya shilingi kusaidia kutimiza azma ya ununuzi wa gari aina ya Coster, litakalosaidia katika usafiri wa pamoja wa wafanyakazi wa afya kwa shughuli mbalimbali. "Tumeguswa na dhamira ya watumishi wetu wa afya kutafuta suluhisho la changamoto zao kupitia harambee. Kama SOYA ONE LIMITED, hatukusita kushiriki kwa moyo mmoja kwa sa...

SOYA ONE LIMITED YAENDELEA KUNG’ARA KATIKA UDHAMINI WA ELIMU NA JAMII TARIME

Image
  Pichani Ni Mkurugenzi wa Soya One Limited ndg Chacha Soya akiwa na viongozi wa serikali Tarime, Mei 20, 2025 – Kampuni ya Soya One Limited inaendelea kudhihirisha dhamira yake ya dhati ya kusaidia jamii kupitia mchango wake mkubwa kwa shule na taasisi za kidini wilayani Tarime, ikiwa ni sehemu ya kaulimbiu yake ya “Jamii Kwanza.” Katika hatua hii kampuni hiyo imetoa gunia 10 za mahindi kwa shule za msingi Sabasaba, Mapinduzi na Azimio, kwa ajili ya chakula kwa wanafunzi. Pia, imeshughulikia gharama za kuunganishiwa umeme katika shule hizo tatu kwa kiasi cha Shilingi 836,577.52, hatua inayolenga kuboresha mazingira ya kujifunzia na kuongeza ufaulu. Kwa kuguswa na hali ya mwanafunzi mmoja mwenye changamoto ya kifedha, kampuni hiyo imetoa Shilingi 100,000 kumuwezesha kupata mahitaji muhimu ya shule na kuendelea na masomo bila vikwazo. Soya One Limited pia imeelekeza msaada wake kwa Shule ya Msingi Magufuli ya watoto wenye mahitaji maalum kwa kutoa gunia tano za mahindi, sukari na ho...

MANCHARE HECHE ATOA MCHANGO WA MILIONI MOJA NA MAJI KATONI 40 KATIKA KIKAO CHA HALMASHAURI KUU CCM TARIME

Image
PICHANI NI MJUMBE MKUTANO MKUU CCM TAIFA NDG MANCHARE HECHE Habari kamili Na Daniel Mussa Tarimee, Mei 19, 2025 Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa, Wakili Manchare Heche, ameendelea kuonesha moyo wa kizalendo na kujitoa kwa ajili ya chama kwa kuchangia kiasi cha shilingi milioni moja pamoja na katoni 40 za maji katika kikao cha Halmashauri Kuu ya CCM Wilaya ya Tarime kilichofanyika jana, Mei 18, 2025, mjini Tarime. Mchango huo umetolewa ikiwa ni sehemu ya kuunga mkono juhudi za chama katika kuimarisha shughuli zake za kisiasa na kiutendaji ndani ya Wilaya ya Tarime. Tukio hilo limepokelewa kwa furaha na pongezi kutoka kwa viongozi mbalimbali wa chama waliohudhuria kikao hicho, wakiongozwa na Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Tarime. Akizungumza na MBC MEDIA mara baada ya kukabidhi msaada huo, Wakili Manchare Heche alisema kuwa anafanya hayo yote kwa lengo la kulisapoti Chama Cha Mapinduzi (CCM) ili liendelee kuimarika na kuleta maendeleo kwa wananchi. Aidha, amepongeza...

Katibu Mkuu Eliakimu Chacha Maswi Achangia Milioni Moja Kufanikisha Mkutano wa Wajasiriamali Tarime

Image
  Pichani ni katibu mkuu wa katiba na sheria Eliakimu Chacha Maswi Tarime, Mei 16, 2025  Katika kuendelea kuunga mkono juhudi za kuwawezesha wanawake na vijana wajasiriamali nchini, Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria, Mheshimiwa Eliakimu Chacha Maswi, ameonesha mfano wa kuigwa kwa kuchangia shilingi milioni moja (1,000,000) kufanikisha mkutano wa mwezi wa wanawake na vijana wajasiriamali wa Wilaya ya Tarime. Mkutano huo muhimu umeandaliwa na Tanzania Women Chamber of Commerce (TWCC) kupitia ofisi yake ya Wilaya ya Tarime, na kufanyika katika ukumbi wa kisasa wa BlueSky, uliopo mjini Tarime. Tukio hilo limekusanya zaidi ya washiriki 150 kutoka kata mbalimbali za Wilaya ya Tarime, ambao ni wanawake na vijana wanaojihusisha na shughuli za ujasiriamali katika sekta tofauti kama vile kilimo, biashara ndogondogo, ushonaji, ufundi na utengenezaji wa bidhaa za mikono. Katika salamu rasmi zilizowasilishwa na mwakilishi wake, Katibu Mkuu Maswi alieleza kuwa mchango wake ni sehemu...

Mdau wa Maendeleo Musa Ryoba Achangia Maji Katika Mkutano wa Wanawake na Vijana Wajasiriamali Tarime

Image
Pichani ni Mkurugenzi wa mwanzo Mpya Ndg Musa Ryoba Tarime, Mei 16, 2025 Mdau wa maendeleo na Mkurugenzi wa Mwanzo Mpya Foundation, Musa Ryoba, ameonesha moyo wa uzalendo na kujitoa kwa jamii kwa kuchangia katoni 20 za maji kwa ajili ya kufanikisha mkutano wa mwezi wa wanawake na vijana wajasiriamali wa Wilaya ya Tarime. Mkutano huo muhimu umeandaliwa na taasisi ya Tanzania Women Chamber of Commerce (TWCC) na kufanyika leo katika ukumbi wa BlueSky, ukiwaleta pamoja wanawake na vijana walioko kwenye sekta mbalimbali za ujasiriamali kwa lengo la kujifunza, kubadilishana uzoefu na kujengewa uwezo wa kukuza biashara zao. Katika mchango wake, Musa Ryoba alisisitiza umuhimu wa kuwainua wanawake na vijana kupitia fursa za kiuchumi na elimu ya ujasiriamali. “Nimeguswa na jitihada za TWCC katika kuwawezesha wanawake na vijana, ndiyo maana niliona ni vyema kuunga mkono mkutano huu. Maji ni kitu kidogo lakini muhimu sana katika mazingira ya mkutano,” alisema. Mratibu wa mkutano huo kutoka TWCC al...

Matiko Foundation Yachangia Shilingi Laki Tano Katika Mkutano wa Wanawake na Vijana Wajasiriamali Tarime

Image
PICHANI NI KATIBU WA MATIKO FOUNDATION PETER MAGWI Tarime, Mei 16, 2025 – Taasisi ya kijamii ya Matiko Foundation imeendelea kudhihirisha dhamira yake ya kusaidia maendeleo ya jamii kwa kuchangia shilingi 500,000 kufanikisha mkutano wa wanawake na vijana wajasiriamali Wilaya ya Tarime, uliofanyika leo chini ya uratibu wa Tanzania Women Chamber of Commerce (TWCC). Mchango huo umetolewa rasmi na Katibu wa Matiko Foundation, Ndg. Peter Magwi, kwa niaba ya taasisi hiyo, ambapo aliipongeza TWCC kwa kuwaunganisha wanawake na vijana katika harakati za kujitegemea kiuchumi. Ndg. Peter Magwi alisema: "Matiko Foundation inatambua umuhimu wa kuwainua wanawake na vijana katika kila hatua ya maendeleo. Tunaamini kuwa kingamano ili ni chachu ya kuinua maisha ya washiriki wa mkutano huu." Mkutano huo umehudhuriwa na washiriki kutoka maeneo mbalimbali ya Wilaya ya Tarime huku Mgeni rasmi akiwa ni Mhe Mkuu wa Wilaya ya Tarime Meja Edward Gowele, ambapo wamepatiwa mafunzo juu ya mbinu bora za ...

Deo Meck Achangia Vifaa Katika Mkutano wa Wanawake na Vijana Wajasiriamali Tarime

Image
  Pichani ni mdau wa maendeleo Deo Meck Tarime, Mei 16, 2025 – Mdau wa maendeleo wa Wilaya ya Tarime, Deo Meck, ameonyesha moyo wa kujitoa kwa jamii kwa kuchangia vifaa muhimu kufanikisha mkutano wa wanawake na vijana wajasiriamali uliofanyika leo mjini Tarime. Katika mchango wake, Deo Meck ametoa dozen 18 za notebook na box 4 za kalamu, vifaa ambavyo vimetumika moja kwa moja katika mkutano huo ulioratibiwa na Tanzania Women Chamber of Commerce (TWCC). Mkutano huo umejikita katika kuwajengea uwezo wanawake na vijana wajasiriamali, kuwaunganisha na fursa za kiuchumi, mitaji na elimu ya ujasiriamali kwa ajili ya kukuza biashara zao. Akizungumza wakati wa hafla ya utoaji wa vifaa hivyo, Deo Meck alisema: "Ninaamini kuwa maendeleo ya jamii yanaanza kwa kuwawezesha wanawake na vijana. Mchango huu ni sehemu ya dhamira yangu ya kusaidia juhudi zao." Uongozi wa TWCC umeushukuru mchango huo na kumpongeza Deo Meck kwa kujitokeza kuwasaidia vijana na wanawake kwa vitendo. Mkutano huo um...

TAASISI YA MARAFIKI WA MAENDELEO TARIME YAMWAGA VIFAA VYA TAALUMA VYENYE THAMANI YA MILIONI 40 KWA SHULE MBILI TARIME VIJIJINI

Image
    Na Daniel Mussa – Tarime Kwa lengo la kuunga mkono juhudi za kuinua kiwango cha elimu katika Wilaya ya Tarime Vijijini, Taasisi ya Marafiki wa Maendeleo Tarime imekabidhi vifaa vya kisasa vya kufundishia na kujifunzia vyenye thamani ya jumla ya shilingi milioni 40 kwa shule mbili za sekondari — Magoto na Mbogi. Kila shule imenufaika na kompyuta za mezani (desktop) mbili, kompyuta mpakato (laptop) moja kwa matumizi ya Mkuu wa Shule, na mashine moja ya kupiga nakala (photocopy machine) aina ya Canon. Vifaa hivyo vimepokelewa kwa furaha kubwa na walimu, wanafunzi na jamii inayozunguka shule hizo. Akikabidhi vifaa hivyo kwa niaba ya taasisi, Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Marafiki wa Maendeleo Tarime, Ndugu Martine Marwa, aliishukuru bodi ya taasisi hiyo pamoja na wadau mbalimbali waliotoa michango yao kwa moyo wa uzalendo. “Tunaishukuru bodi ya taasisi yetu kwa kuratibu na kufanikisha upatikanaji wa vifaa hivi kupitia michango ya wadau wetu. Tunaamini kwamba uwekezaji katika e...

RAYMOND JOHN OLE MATINDA ATETA NA KAMATI TENDAJI YA JUMUIYA YA WAZAZI CCM TARIME

Image
Ajadili Mpango wa Kujenga Nyumba ya Katibu wa Jumuiya TARIME, Aprili 30, 2025 — Katibu wa Jumuiya ya Wazazi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Tarime, Ndugu Raymond John Ole Matinda, amekutana na Kamati Tendaji ya jumuiya hiyo kwa kikao maalum kilicholenga kujadili mpango wa kujenga nyumba ya Katibu wa Jumuiya hiyo. Akizungumza na MBC MEDIA mara baada ya kikao hicho, Raymond amesema kuwa lengo kuu la kikao lilikuwa ni kuweka msingi wa mpango huo muhimu, ambao una dhamira ya kuboresha mazingira ya kazi kwa kiongozi mkuu wa jumuiya hiyo wilayani Tarime. "Tulikaa kikao cha Kamati Tendaji ambapo tulijadili kwa kina suala la ujenzi wa nyumba ya Katibu wa Jumuiya. Hili ni jambo la msingi katika kuimarisha utendaji kazi wa jumuiya yetu," alisema Raymond. Alibainisha kuwa hatua hiyo ni mwanzo wa mchakato wa muda mrefu wa kuhakikisha jumuiya ya wazazi inakuwa na miundombinu bora inayowezesha viongozi wake kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi. "Tumeamua kuanza kwa kuweka maono ...

KADA WA CCM NDG. DEO MECK AWEZESHA UPATIKANAJI WA ZAIDI YA MILIONI 5.8 KATIKA HARAMBEE YA UJENZI WA KANISA LA WASABATO MTENYO – TARIME

Image
Pichani ni Kada Wa chama Cha Mapinduzi (CCM) Ndg DEO MECK  Tarime, Mara – Aprili 19, 2025 Katika kuunga mkono juhudi za maendeleo ya kiroho na kijamii, Kada maarufu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Ndg. Deo Meck, amewezesha upatikanaji wa kiasi cha shilingi milioni 5.869,900 katika harambee ya kuchangia ujenzi wa Kanisa la Waadventista Wasabato Mtenyo, lililopo Kata ya Kenyamanyori, Halmashauri ya Mji wa Tarime. Katika harambee hiyo, Ndg. Deo Meck hakuhudhuria binafsi, lakini aliwakilishwa na Paschal Maswi Waryoba, ambaye alitoa mchango huo mkubwa kwa niaba yake, na kusisitiza dhamira ya Meck ya kuendelea kushirikiana na jamii katika shughuli zote za maendeleo, bila kujali itikadi au tofauti za kidini. Harambee hiyo ilifanyika kwa hamasa kubwa na kuhudhuriwa na waumini wa dhehebu hilo, viongozi wa dini, wakazi wa eneo hilo pamoja na wageni waalikwa mbalimbali walioungana kwa pamoja kuchangia maendeleo ya kiroho kwa vitendo. Akizungumza kwa niaba ya Meck, Paschal Maswi Waryoba alisema:...

SOYA ONE LIMITED Yaendelea Kuthibitisha Kauli Mbiu Yake “Jamii Kwanza” – Mkurugenzi Chacha Soya Aahidi Motisha ya Kila Goli kwa Bomani FC

Image
PICHANI NI MKURUGENZI WA SOYA ONE LIMITED (CHACHA SOYA) Tarime, Aprili 17, 2025 Katika kuunga mkono juhudi za Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika kuinua sekta ya michezo nchini, Mkurugenzi wa SOYA ONE LIMITED, Mheshimiwa Chacha Soya, ameahidi motisha kabambe kwa timu ya Bomani FC. Katika mechi muhimu inayotarajiwa kuchezwa leo dhidi ya Ketare FC, Mheshimiwa Chacha Soya ameahidi kutoa kiasi cha shilingi 100,000 kwa kila goli litakalofungwa na timu ya Bomani endapo watashinda mechi hiyo. Hatua hiyo imelenga kuinua morali ya vijana na kuhimiza ushindani wa kweli kwenye mashindano ya soka ngazi ya jamii. Hii ni sehemu ya mpango mpana wa kampuni hiyo kuwekeza kwenye maendeleo ya kijamii kupitia michezo, kama njia ya kukuza vipaji na kujenga mshikamano. Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan  "Tunaunga mkono kwa dhati juhudi za Mheshimiwa Rais katika kuibadilisha tasnia ya michezo kuwa chombo cha maendeleo ya kiuchumi na kijamii. Kama kampu...