MKURUGENZI WA SOYA ONE LIMITED AWASISITIZA WAUMINI WA EAGT RONSOTI TARIME MJINI KUILINDA AMANI; AFANIKISHA UPATIKANAJI WA MCHANGO WA MILIONI 12, ACHANGIA MILIONI 8 NA ASINDIKIZWA KWA MILIONI 5

MKURUGENZI WA SOYA ONE LIMITED 
(CHACHA GESORA)

 Tarime Mjini, Tanzania – Mkurugenzi wa Soya One Limited, Chacha Soya, ameendelea kuonyesha moyo wa kujitoa kwa jamii baada ya kufanikisha upatikanaji wa mchango wa jumla ya shilingi milioni 12, ambapo mwenyewe alichangia milioni 8, na waumini pamoja na wageni wengine wakasindikiza kwa milioni 5.


Mkurugenzi huyo alialikwa rasmi kama mgeni maalum katika ibada ya Jumapili iliyofanyika katika Kanisa la EAGT Ronsoti, ibada iliyojaa uwepo wa Mungu na iliyoongozwa na Mchungaji Maswi.


Katika hotuba yake yenye kugusa mioyo, Mkurugenzi Soya alisisitiza umuhimu wa kulinda amani ya nchi akisema:



“Amani yetu ni nguzo ya maendeleo. Tanzania imebarikiwa na Mungu kwa utulivu wake. Tuilinde, tuiombee, na tuishi kama watu wanaothamini urithi huu adhimu.”

Alisisitiza kuwa amani ndiyo msingi wa ibada, biashara, uchumi na ustawi wa familia, hivyo kila Mwanatarime na Mtanzania kwa ujumla ana wajibu wa kuwa mlinzi wa amani.

Katika kuendelea kusapoti kazi ya Mungu na jamii, Mkurugenzi wa Soya One Limited aliunga mkono kanisa hilo kwa kuchangia milioni 8, na waumini pamoja na wageni wengine wakasindikiza kwa kuongeza milioni 5, hatua iliyowafanya waumini kushukuru na kumpongeza kwa moyo wake wa ukarimu na uongozi wa mfano.


Mchungaji Maswi, akipokea mchango huo,alisema:

MCHUNGAJI MASWI KANISA LA EAGT RONSOTI TARIME MJINI 

“Tunamshukuru Mkurugenzi Soya kwa moyo wake wa upendo. Huduma ya injili inaendelea kusimama kwa sababu ya watu kama yeye. Mungu azidi kumuinua.”

Kwa upande wake, Mkurugenzi Soya alisisitiza kuwa kaulimbiu ya kampuni yake, “Jamii Kwanza,” itaendelea kuwa dira ya kusaidia kanisa, vijana, na jamii ya Tarime kwa ujumla.


Ibada ilihitimishwa kwa maombi maalum ya kuliombea taifa, viongozi wetu, na shughuli za maendeleo, pamoja na kumbariki mgeni rasmi kwa kujitoa kwake kwa moyo wa kipekee. alisema:

“Tunamshukuru Mkurugenzi Soya kwa moyo wake wa upendo. Huduma ya injili inaendelea kusimama kwa sababu ya watu kama yeye. Mungu azidi kumuinua.”

Kwa upande wake, Mkurugenzi Soya alisisitiza kuwa kaulimbiu ya kampuni yake, “Jamii Kwanza,” itaendelea kuwa dira ya kusaidia kanisa, vijana, na jamii ya Tarime kwa ujumla.


Ibada ilihitimishwa kwa maombi maalum ya kuliombea taifa, viongozi wetu, na shughuli za maendeleo, pamoja na kumbariki mgeni rasmi kwa kujitoa kwake kwa moyo wa kipekee.


Comments

Popular posts from this blog

GWAJIMA AACHE KUCHEZEA AMANI YA TAIFA, NA MHE. RAIS SAMIA AANGALIE JICHO LA CHINI YA KIVULI HIKI

SOYA ONE LIMITED YAENDELEA KUNG’ARA KATIKA UDHAMINI WA ELIMU NA JAMII TARIME