SOYA ONE LIMITED YAIPONGEZA SERIKALI KWA KUWAWEZESHA WACHIMBAJI WADOGO NA KUIUNGA MKONO SEKTA YA MADINI

PICHANI NI MKURUGENZI WA SOYA ONE LIMITED NDG CHACHA SOYA

MUSOMA, JUNI 7, 2025 Kampuni ya Soya One Limited imetoa pongezi za dhati kwa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa hatua madhubuti inazochukua katika kuwawezesha na kuwashika mkono wachimbaji wadogo wadogo wa madini nchini, hususan katika mkoa wa Mara.


Akizungumza mara baada ya kukamilika kwa kongamano kubwa la wachimbaji wa madini wa Mkoa wa Mara lililofanyika tarehe 6 Juni 2025 katika viwanja vya Mkendo, Musoma Mjini, Mkurugenzi wa Soya One Limited, Ndugu Chacha Soya, amesema kuwa mafanikio ya sekta ya madini yanaakisi juhudi za serikali ya awamu ya sita katika kuhakikisha wachimbaji wadogo wanapewa mazingira bora ya kufanya kazi kwa tija na usalama.


"Natoa shukrani za dhati kwa Serikali kwa kuendelea kutambua mchango wa wachimbaji wadogo, lakini zaidi kwa hatua ya kuwajengea uwezo na kuwawekea mazingira rafiki ya kuchangia pato la taifa," alisema Ndugu Chacha Soya. "Sisi kama Soya One Limited, tunaiona fursa hii kama wito wa kuongeza ushirikiano wetu na serikali pamoja na kuendelea kuwa mstari wa mbele katika kuchangia maendeleo ya jamii kupitia sekta ya madini."


Katika kongamano hilo, Soya One Limited ilipatiwa cheti maalum cha shukrani kutoka Ofisi ya Madini Mkoa wa Mara, ikiwa ni kutambua mchango wa kampuni hiyo kama mdau muhimu aliyefanikisha uandaaji na utekelezaji wa kongamano hilo. Akipokea cheti hicho kwa niaba ya kampuni, Mkurugenzi huyo alieleza kuwa ni ishara ya ushirikiano mzuri kati ya sekta binafsi na serikali.


"Naipongeza Ofisi ya Madini Mkoa wa Mara kwa kututambua kupitia cheti hiki cha shukrani. Hili ni jambo kubwa kwetu kama kampuni, linaonesha kuwa juhudi zetu katika kuunga mkono sekta hii zinathaminiwa," aliongeza Chacha.


Aidha, Mkurugenzi huyo alitumia nafasi hiyo kumpongeza Waziri wa Madini, Mheshimiwa Anthony Mavunde, kwa kuwaongoza kwa weledi wadau wa madini na kuonesha mwelekeo mpya wa mageuzi chanya katika sekta hiyo. Vilevile, alitoa pongezi kwa Mkuu wa Mkoa wa Mara, Kanali Evans Mtambi, kwa kazi nzuri ya kusimamia na kuratibu maendeleo ya sekta ya madini ndani ya mkoa.


"Kongamano hili ni ushahidi kuwa mkoa wa Mara uko kwenye kasi ya maendeleo. Tunaipongeza ofisi ya Mkuu wa Mkoa kwa uongozi bora unaoleta tija na mshikamano miongoni mwa wadau," alisema Mkurugenzi huyo.


Soya One Limited ni kampuni inayojihusisha na shughuli za uchimbaji wa madini na imekuwa mstari wa mbele kusaidia jamii na kuunga mkono juhudi za serikali chini ya kaulimbiu yao "Jamii Kwanza."

Comments

Popular posts from this blog

GWAJIMA AACHE KUCHEZEA AMANI YA TAIFA, NA MHE. RAIS SAMIA AANGALIE JICHO LA CHINI YA KIVULI HIKI

MKURUGENZI WA SOYA ONE LIMITED AWASISITIZA WAUMINI WA EAGT RONSOTI TARIME MJINI KUILINDA AMANI; AFANIKISHA UPATIKANAJI WA MCHANGO WA MILIONI 12, ACHANGIA MILIONI 8 NA ASINDIKIZWA KWA MILIONI 5

SOYA ONE LIMITED YAENDELEA KUNG’ARA KATIKA UDHAMINI WA ELIMU NA JAMII TARIME