SOYA ONE LIMITED YAENDELEA KUNG’ARA KATIKA UDHAMINI WA ELIMU NA JAMII TARIME

 

Pichani Ni Mkurugenzi wa Soya One Limited ndg Chacha Soya akiwa na viongozi wa serikali


Tarime, Mei 20, 2025 – Kampuni ya Soya One Limited inaendelea kudhihirisha dhamira yake ya dhati ya kusaidia jamii kupitia mchango wake mkubwa kwa shule na taasisi za kidini wilayani Tarime, ikiwa ni sehemu ya kaulimbiu yake ya “Jamii Kwanza.”

Katika hatua hii kampuni hiyo imetoa gunia 10 za mahindi kwa shule za msingi Sabasaba, Mapinduzi na Azimio, kwa ajili ya chakula kwa wanafunzi. Pia, imeshughulikia gharama za kuunganishiwa umeme katika shule hizo tatu kwa kiasi cha Shilingi 836,577.52, hatua inayolenga kuboresha mazingira ya kujifunzia na kuongeza ufaulu.

Kwa kuguswa na hali ya mwanafunzi mmoja mwenye changamoto ya kifedha, kampuni hiyo imetoa Shilingi 100,000 kumuwezesha kupata mahitaji muhimu ya shule na kuendelea na masomo bila vikwazo.

Soya One Limited pia imeelekeza msaada wake kwa Shule ya Msingi Magufuli ya watoto wenye mahitaji maalum kwa kutoa gunia tano za mahindi, sukari na homo, huku ikikumbuka pia watoto wanaolelewa Msikiti wa Jamia Tarime kwa kuwachangia gunia sita za mahindi.

Akizungumza wakati wa hafla ya makabidhiano, Mkurugenzi wa Soya One Limited, Bw. Chacha Soya, aliipongeza Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania chini ya uongozi wa Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kazi kubwa ya kusimamia maendeleo na ustawi wa wananchi.

> “Mheshimiwa Rais ameendelea kuwa nguzo ya matumaini kwa Watanzania kupitia uongozi wake madhubuti na wa huruma. Sisi kama Soya One Limited tunaahidi kuendelea kuiunga mkono jamii sambamba na juhudi za Serikali katika kuleta maendeleo ya kweli,” alisema Bw. Soya.













Wananchi, viongozi wa shule, na viongozi wa dini wameipongeza kampuni hiyo kwa moyo wa kujitoa na mchango wake mkubwa kwa jamii. Wametoa wito kwa wadau wengine kujifunza kutoka kwa Soya One Limited ili pamoja wajenge jamii imara, yenye haki na usawa kwa wote.

Kwa msaada huu, Soya One Limited inaendelea kujijenga kama kampuni ya mfano katika uwajibikaji wa kijamii na mshirika wa maendeleo ya Tanzania.


Comments

Popular posts from this blog

GWAJIMA AACHE KUCHEZEA AMANI YA TAIFA, NA MHE. RAIS SAMIA AANGALIE JICHO LA CHINI YA KIVULI HIKI

MKURUGENZI WA SOYA ONE LIMITED AWASISITIZA WAUMINI WA EAGT RONSOTI TARIME MJINI KUILINDA AMANI; AFANIKISHA UPATIKANAJI WA MCHANGO WA MILIONI 12, ACHANGIA MILIONI 8 NA ASINDIKIZWA KWA MILIONI 5