Jackson Kangoye Atoa Mchango wa Milioni 2 kwa Watendaji Tarime, Aahidi Kuwapa Laptop Kila Kata
Tarime, Tanzania – Kada wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na mdau wa maendeleo, Jackson Kangoye, ameonesha moyo wa uzalendo kwa kuchangia shilingi milioni 2 kwenye mfuko wa watendaji wa Halmashauri ya Mji wa Tarime (Watendaji Fund).
Akizungumza wakati wa hafla ya makabidhiano ya mchango huo, Kangoye alisema lengo lake ni kuwaunga mkono watendaji katika utekelezaji wa majukumu yao kwa ufanisi zaidi. Aidha, alitangaza kuwa atatoa kompyuta mpakato (laptop) kwa kila kata katika mji wa Tarime, hatua inayolenga kuboresha utendaji kazi wa watendaji wa kata na kuimarisha mifumo ya utawala.
“Nafahamu changamoto wanazokutana nazo watendaji wetu, hasa katika upatikanaji wa vifaa vya kiteknolojia. Nimeamua kuwapatia laptop kwa kila kata ili kurahisisha kazi zao na kuongeza ufanisi katika kuhudumia wananchi,” alisema Kangoye.
Watendaji wamepokea mchango huo kwa shukrani kubwa, wakisema hatua hiyo itasaidia kuboresha utendaji kazi na kuwapa motisha katika kutimiza majukumu yao.
Jackson Kangoye ameendelea kuwa mdau muhimu wa maendeleo katika mji wa Tarime, akishiriki katika miradi mbalimbali ya kijamii kwa lengo la kuboresha maisha ya wananchi.

.jpeg)




Comments
Post a Comment