BULAYA AUNGANA NA VIJANA BODA BODA, ATOA MSAADA NA KUHIMIZA AMANI

                            PICHANI NI 
MHE. ESTHER BULAYA AKIWA NA MAAFISA USAFILISHAJI WA BUNDA STOO

Na mwandishi wetu Bunda mjini

 Mbunge wa Jimbo la Bunda Mjini, Esther Bulaya, ametembelea vijana wa kituo cha bodaboda Bunda Stoo na kushiriki nao mazungumzo yenye kujenga mshikamano na maendeleo ya vijana.

Katika ziara hiyo, Mhe. Bulaya alionyesha kuguswa na hali ya kijiwe chao na kutoa msaada wa kiasi cha shilingi 250,000 kwa ajili ya ukarabati, ili kuboresha mazingira yao na kupata kivuli bora wakati wa shughuli zao za kila siku.

Bulaya akiteta na maafisa usafilishaji

Aidha, alimsaidia kijana mmoja kwa kumpatia fedha za kufanya marekebisho ya pikipiki yake, akilenga kuongeza usalama barabarani na kuboresha kipato chake kupitia kazi ya usafirishaji.

Mbali na misaada hiyo, Mhe. Bulaya alitoa elimu na mawaidha kwa vijana hao, akiwataka kuwa makini na watu wanaoweza kuwatumia vibaya kwa maslahi binafsi. Aliwakumbusha madhara ya kushiriki katika vitendo vya machafuko, akirejea matukio yaliyojitokeza wakati wa uchaguzi wa Tanzania General Election 2025, na kusisitiza umuhimu wa kulinda amani na utulivu.

Katika hotuba yake, pia aliwahamasisha vijana kuendelea kufanya kazi kwa bidii na kutumia fursa mbalimbali zinazotolewa na serikali chini ya uongozi wa Rais, Samia Suluhu Hassan, ambaye ameendelea kuweka mazingira rafiki kwa maendeleo ya vijana nchini.

Ziara hiyo imeacha faraja kubwa kwa vijana wa bodaboda Bunda Stoo, ambao wameahidi kuendelea kushirikiana na viongozi wao katika kuleta maendeleo na kudumisha amani katika jamii.






Comments

Popular posts from this blog

GWAJIMA AACHE KUCHEZEA AMANI YA TAIFA, NA MHE. RAIS SAMIA AANGALIE JICHO LA CHINI YA KIVULI HIKI

MKURUGENZI WA SOYA ONE LIMITED AWASISITIZA WAUMINI WA EAGT RONSOTI TARIME MJINI KUILINDA AMANI; AFANIKISHA UPATIKANAJI WA MCHANGO WA MILIONI 12, ACHANGIA MILIONI 8 NA ASINDIKIZWA KWA MILIONI 5

SOYA ONE LIMITED YAENDELEA KUNG’ARA KATIKA UDHAMINI WA ELIMU NA JAMII TARIME