MKURUGENZI WA SOYA ONE LIMITED ASHIRIKI MAZISHI YA MHANDISI GISIMA NYAMHANGA BUNDA MJINI, ATOA SALAMU ZA POLE KWA FAMILIA NA SHIRIKA LA UMEME TANZANIA
Na Daniel Mussa – Bunda Mkurugenzi wa kampuni ya SOYA ONE LIMITED, Bw. Chacha Soya, ameshiriki mazishi ya aliyekuwa Mhandisi wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), marehemu Gisima Nyamhanga, yaliyofanyika leo katika mtaa wa Migungani, Bunda Mjini, mkoani Mara. Pichani ni Mkurugenzi wa SOYA ONE LIMITED (CHACHA SOYA) Katika tukio hilo la majonzi lililojumuisha mamia ya waombolezaji, viongozi wa serikali, wawakilishi wa TANESCO na wakazi wa Bunda, Bw. Chacha Soya alitoa salamu za pole kwa familia ya marehemu pamoja na shirika la TANESCO kwa kumpoteza mmoja wa watumishi wake waaminifu. Kauli Rasmi ya Bw. Chacha Soya : > “Kifo cha Mhandisi Gisima Nyamhanga ni pigo kubwa kwa sekta ya nishati nchini. Ameacha alama kubwa kupitia weledi, uadilifu na moyo wake wa kujitolea. Kwa niaba ya SOYA ONE LIMITED, natoa pole za dhati kwa familia yake, ndugu, marafiki na shirika la TANESCO. Tuko nanyi katika kipindi hiki kigumu, na tunawaombea faraja, nguvu na amani.” Akiwa mmoja wa wadau wa maen...