Mjumbe wa Baraza Kuu UWT Taifa Rhobi Samwel Achangia Shilingi Laki Tano kwa Ujenzi wa Msikiti wa BAKWATA Tarime
Tarime, 31 Machi 2025 – Mjumbe wa Baraza Kuu la Umoja wa Wanawake wa Chama Cha Mapinduzi (UWT) Taifa, Mheshimiwa Rhobi Samwel, ameonesha moyo wa ukarimu kwa kuchangia shilingi 500,000 kwa ajili ya ujenzi wa Msikiti wa BAKWATA uliopo Tarime Mjini.
Mchango huo ulitolewa jana, tarehe 30 Machi 2025, kupitia mwakilishi wake Idd Hussein, ambaye alisisitiza dhamira ya Mheshimiwa Rhobi katika kusaidia shughuli za kijamii na maendeleo ya kidini.
Akizungumza kwa niaba ya Mheshimiwa Rhobi, Idd Hussein aliwahimiza waumini wa Kiislamu na jamii kwa ujumla kuendelea kushirikiana ili kuhakikisha ujenzi wa msikiti huo unakamilika kwa wakati.
Viongozi wa BAKWATA Tarime walipokea mchango huo kwa shukrani kubwa, wakisema ni hatua muhimu katika kufanikisha mradi huo wa ujenzi. Michango zaidi inaendelea kukusanywa kutoka kwa wadau mbalimbali ili kuhakikisha msikiti huo unakamilika na kuanza kutumika.
Kwa mawasiliano zaidi au kama unahabari
Piga +255656114499
Daniel Yohana Mussa
.jpeg)
Comments
Post a Comment