SOYA ONE LTD. YAMLILIA MAREHEMU BI. MARTINA CHAMBIRI – MKURUGENZI CHACHA SOYA AFUNGUKA

       Pichani ni Mkurugenzi wa SOYA ONE                       LIMITED (Chacha Soya)

Tarime, Mara – Machi 13, 2025 – Kampuni ya uchimbaji dhahabu, Soya One Limited, imetoa salamu za pole kwa familia ya marehemu Bi. Martina Chambiri, ambaye amezikwa leo Machi 13, 2025, katika Kata ya Bomani, Tarime Mjini, baada ya kuaga dunia hivi karibuni.

Akizungumza baada ya mazishi, Mkurugenzi wa Soya One Limited, Chacha Soya, alisema kifo cha Bi. Martina ni pigo kubwa kwa familia yake na jamii nzima ya Tarime. "Tumempoteza mtu muhimu sana, mwenye hekima na upendo. Alikuwa mshauri na mlezi wa wengi. Tunasikitika sana kwa kuondokewa naye, lakini tunamwombea apumzike kwa amani," alisema kwa masikitiko.

Picha ya Mwili wa MAREHEMU Bi. Martina Chambiri ukiwa unaagwa

Mazishi ya marehemu yamefanyika leo Kata ya Bomani, Tarime Mjini, yakiwa yamehudhuriwa na ndugu, marafiki, na watu mbalimbali walioguswa na maisha yake.

Chacha Soya aliwahakikishia wanafamilia kuwa Soya One Limited ipo pamoja nao na itaendelea kuwaunga mkono katika kipindi hiki kigumu. "Tunawaombea faraja wanafamilia wote, Mungu awape nguvu," aliongeza.

Marehemu Bi. Martina Chambiri atakumbukwa kwa mchango wake mkubwa kwa familia na jamii. Mungu ailaze roho yake mahali pema peponi.

Comments

Popular posts from this blog

GWAJIMA AACHE KUCHEZEA AMANI YA TAIFA, NA MHE. RAIS SAMIA AANGALIE JICHO LA CHINI YA KIVULI HIKI

MKURUGENZI WA SOYA ONE LIMITED AWASISITIZA WAUMINI WA EAGT RONSOTI TARIME MJINI KUILINDA AMANI; AFANIKISHA UPATIKANAJI WA MCHANGO WA MILIONI 12, ACHANGIA MILIONI 8 NA ASINDIKIZWA KWA MILIONI 5

SOYA ONE LIMITED YAENDELEA KUNG’ARA KATIKA UDHAMINI WA ELIMU NA JAMII TARIME