MKUU WA WILAYA YA TARIME MEJA EDWARD GOWELE AFANYA ZIARA ITIRYO, AWAPONGEZA WANANCHI KWA KUCHANGIA MAENDELEO
Mkuu wa Wilaya ya Tarime meja Edward gowele
Tarime, Mara – Mkuu wa Wilaya ya Tarime, Meja Edward Gowele, amefanya ziara katika Kijiji cha Itiryo, Tarime Vijijini, ambapo amewapongeza wananchi kwa kujitolea katika miradi ya maendeleo.
Akizungumza na wananchi wa kijiji hicho, Meja Gowele aliwasifu kwa mshikamano wao katika kuboresha huduma za kijamii kama elimu, afya na miundombinu. Alisema kuwa juhudi hizo zinaonyesha uzalendo na mshikamano wa dhati katika kuleta maendeleo ya kweli.
Wananchi Wa Kijiji Cha Itiryo"Nawapongeza kwa moyo huu wa kujitolea. Maendeleo hayawezi kuletwa na serikali pekee, lakini kwa kushirikiana, tunaweza kufanikisha mambo makubwa," alisema.
Katika hotuba yake, Meja Gowele pia alimtaja na kumpongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, kwa jitihada zake za kuleta maendeleo katika kila kona ya nchi. Alisema kuwa kupitia uongozi wake thabiti, serikali inaendelea kutekeleza miradi mikubwa ya maendeleo inayogusa maisha ya wananchi moja kwa moja.
"Rais wetu Mama Samia ameendelea kusogeza maendeleo kila kona ya nchi, na sisi viongozi wa ngazi za chini tunatekeleza maono yake kwa kushirikiana na wananchi," aliongeza.
Rais Samia Suluhu HassaWananchi wa Itiryo walimshukuru Mkuu wa Wilaya kwa kutembelea kijiji chao na kuahidi kuendelea kushirikiana na serikali katika kuboresha hali ya maisha yao.
Ziara hiyo ni sehemu ya mwendelezo wa mikakati ya serikali kuhakikisha maendeleo yanawafikia wananchi wa maeneo yote ya Tarime Vijijini.



Comments
Post a Comment