MANCHARE HECHE ATOA MCHANGO WA MILIONI MOJA NA MAJI KATONI 40 KATIKA KIKAO CHA HALMASHAURI KUU CCM TARIME

PICHANI NI MJUMBE MKUTANO MKUU CCM TAIFA NDG MANCHARE HECHE


Habari kamili Na Daniel Mussa

Tarimee, Mei 19, 2025 Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa, Wakili Manchare Heche, ameendelea kuonesha moyo wa kizalendo na kujitoa kwa ajili ya chama kwa kuchangia kiasi cha shilingi milioni moja pamoja na katoni 40 za maji katika kikao cha Halmashauri Kuu ya CCM Wilaya ya Tarime kilichofanyika jana, Mei 18, 2025, mjini Tarime.


Mchango huo umetolewa ikiwa ni sehemu ya kuunga mkono juhudi za chama katika kuimarisha shughuli zake za kisiasa na kiutendaji ndani ya Wilaya ya Tarime. Tukio hilo limepokelewa kwa furaha na pongezi kutoka kwa viongozi mbalimbali wa chama waliohudhuria kikao hicho, wakiongozwa na Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Tarime.


Akizungumza na MBC MEDIA mara baada ya kukabidhi msaada huo, Wakili Manchare Heche alisema kuwa anafanya hayo yote kwa lengo la kulisapoti Chama Cha Mapinduzi (CCM) ili liendelee kuimarika na kuleta maendeleo kwa wananchi.


Aidha, amepongeza Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kazi nzuri na iliyo tukuka ya kuwaletea Watanzania maendeleo, akisema kuwa uongozi wa Rais umekuwa wa mfano na unapaswa kuungwa mkono na kila mmoja.


"Chama chetu kinahitaji mshikamano, moyo wa kujitolea na mshirikiano wa kweli. Nimeguswa kuchangia kwa kadri ya uwezo wangu kama sehemu ya kuonesha mapenzi yangu kwa CCM na wananchi wa Tarime," alisema Manchare.


Kwa upande wao, viongozi wa CCM Wilaya ya Tarime wamemshukuru Wakili Manchare Heche kwa moyo wake wa kizalendo na kuwataka wanachama wengine kuiga mfano huo mzuri wa kujitoa bila kusukumwa.


Kikao hicho cha Halmashauri Kuu ya Wilaya kilifanyika kwa mafanikio makubwa, kikijadili maendeleo ya chama, utekelezaji wa ilani, na mikakati ya kuimarisha ushindi wa CCM katika chaguzi zijazo.


Comments