Matiko Foundation Yachangia Shilingi Laki Tano Katika Mkutano wa Wanawake na Vijana Wajasiriamali Tarime

PICHANI NI KATIBU WA MATIKO FOUNDATION PETER MAGWI

Tarime, Mei 16, 2025 – Taasisi ya kijamii ya Matiko Foundation imeendelea kudhihirisha dhamira yake ya kusaidia maendeleo ya jamii kwa kuchangia shilingi 500,000 kufanikisha mkutano wa wanawake na vijana wajasiriamali Wilaya ya Tarime, uliofanyika leo chini ya uratibu wa Tanzania Women Chamber of Commerce (TWCC).


Mchango huo umetolewa rasmi na Katibu wa Matiko Foundation, Ndg. Peter Magwi, kwa niaba ya taasisi hiyo, ambapo aliipongeza TWCC kwa kuwaunganisha wanawake na vijana katika harakati za kujitegemea kiuchumi.


Ndg. Peter Magwi alisema:

"Matiko Foundation inatambua umuhimu wa kuwainua wanawake na vijana katika kila hatua ya maendeleo. Tunaamini kuwa kingamano ili ni chachu ya kuinua maisha ya washiriki wa mkutano huu."


Mkutano huo umehudhuriwa na washiriki kutoka maeneo mbalimbali ya Wilaya ya Tarime huku Mgeni rasmi akiwa ni Mhe Mkuu wa Wilaya ya Tarime Meja Edward Gowele, ambapo wamepatiwa mafunzo juu ya mbinu bora za biashara, usimamizi wa fedha, na fursa za mikopo kwa wajasiriamali wadogo.

Comments

Popular posts from this blog

GWAJIMA AACHE KUCHEZEA AMANI YA TAIFA, NA MHE. RAIS SAMIA AANGALIE JICHO LA CHINI YA KIVULI HIKI

MKURUGENZI WA SOYA ONE LIMITED AWASISITIZA WAUMINI WA EAGT RONSOTI TARIME MJINI KUILINDA AMANI; AFANIKISHA UPATIKANAJI WA MCHANGO WA MILIONI 12, ACHANGIA MILIONI 8 NA ASINDIKIZWA KWA MILIONI 5

SOYA ONE LIMITED YAENDELEA KUNG’ARA KATIKA UDHAMINI WA ELIMU NA JAMII TARIME