Deo Meck Achangia Vifaa Katika Mkutano wa Wanawake na Vijana Wajasiriamali Tarime

 

Pichani ni mdau wa maendeleo Deo Meck

Tarime, Mei 16, 2025 – Mdau wa maendeleo wa Wilaya ya Tarime, Deo Meck, ameonyesha moyo wa kujitoa kwa jamii kwa kuchangia vifaa muhimu kufanikisha mkutano wa wanawake na vijana wajasiriamali uliofanyika leo mjini Tarime.


Katika mchango wake, Deo Meck ametoa dozen 18 za notebook na box 4 za kalamu, vifaa ambavyo vimetumika moja kwa moja katika mkutano huo ulioratibiwa na Tanzania Women Chamber of Commerce (TWCC).


Mkutano huo umejikita katika kuwajengea uwezo wanawake na vijana wajasiriamali, kuwaunganisha na fursa za kiuchumi, mitaji na elimu ya ujasiriamali kwa ajili ya kukuza biashara zao.


Akizungumza wakati wa hafla ya utoaji wa vifaa hivyo, Deo Meck alisema:

"Ninaamini kuwa maendeleo ya jamii yanaanza kwa kuwawezesha wanawake na vijana. Mchango huu ni sehemu ya dhamira yangu ya kusaidia juhudi zao."


Uongozi wa TWCC umeushukuru mchango huo na kumpongeza Deo Meck kwa kujitokeza kuwasaidia vijana na wanawake kwa vitendo.


Mkutano huo umehudhuriwa pia na wadau wa maendeleo, wawakilishi wa serikali na wanachama wa TWCC kutoka maeneo mbalimbali ya Wilaya ya Tarime.

Comments

Popular posts from this blog

GWAJIMA AACHE KUCHEZEA AMANI YA TAIFA, NA MHE. RAIS SAMIA AANGALIE JICHO LA CHINI YA KIVULI HIKI

MKURUGENZI WA SOYA ONE LIMITED AWASISITIZA WAUMINI WA EAGT RONSOTI TARIME MJINI KUILINDA AMANI; AFANIKISHA UPATIKANAJI WA MCHANGO WA MILIONI 12, ACHANGIA MILIONI 8 NA ASINDIKIZWA KWA MILIONI 5

SOYA ONE LIMITED YAENDELEA KUNG’ARA KATIKA UDHAMINI WA ELIMU NA JAMII TARIME