"KAULI YA DC GOWELE YAPOTOSHWA, HAKUZUIA UCHUNGUZI WA UPOTEVU WA WATU"
Habari Kamili:
Mnamo tarehe 31 Machi 2025, Mkuu wa Wilaya ya Tarime, Meja Edward Gowele, alizungumza katika msiba na kusisitiza umuhimu wa kuheshimu mazingira ya msiba kwa kuwaliza wafiwa zaidi. Alieleza kuwa ni vyema jukwaa la msiba liwe la viongozi wa kiroho, huku viongozi wengine wakitoa maneno ya faraja na pole kwa wafiwa badala ya kugeuza tukio hilo kuwa jukwaa la siasa.
Hata hivyo, mwanachama wa CHADEMA alitumia msiba huo kujaribu kuihusisha serikali na upotevu wa watu kwa kudai kuwa serikali inapaswa kuwaonyesha wananchi makaburi ya waliopotea. Kauli hiyo inaashiria kuwa tayari anaihukumu serikali bila ushahidi na anafanya uchochezi kwa kudhani kwamba waliopotea wameuawa.
DC Gowele alikemea upotoshaji huo, akisisitiza kuwa madai yanapaswa kuwasilishwa kwa ushahidi wa kutosha kupitia vyombo vya sheria badala ya kuzua taharuki kwa wananchi. Alisema kuwa wanasiasa wana nafasi zao za kufanya mikutano ya kisiasa, lakini msiba si mahali pa kuanzisha mjadala wa tuhuma zisizo na msingi.
Taarifa zinazozagaa kwenye mitandao ya kijamii zikidai kuwa DC Gowele alizuia mjadala kuhusu upotevu wa watu ni za upotoshaji. Ukweli ni kwamba alihimiza utulivu, heshima kwa wafiwa, na kuacha kutumia misiba kama majukwaa ya siasa za uchochezi. Serikali inaendelea kuchunguza matukio ya upotevu wa watu, na wananchi wanahimizwa kushirikiana na vyombo vya usalama kwa kutoa taarifa sahihi badala ya kueneza propaganda zisizo na ushahidi.


Comments
Post a Comment