SOYA ONE LIMITED Yaendelea Kuthibitisha Kauli Mbiu Yake “Jamii Kwanza” – Mkurugenzi Chacha Soya Aahidi Motisha ya Kila Goli kwa Bomani FC
Tarime, Aprili 17, 2025
Katika kuunga mkono juhudi za Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika kuinua sekta ya michezo nchini, Mkurugenzi wa SOYA ONE LIMITED, Mheshimiwa Chacha Soya, ameahidi motisha kabambe kwa timu ya Bomani FC.
Katika mechi muhimu inayotarajiwa kuchezwa leo dhidi ya Ketare FC, Mheshimiwa Chacha Soya ameahidi kutoa kiasi cha shilingi 100,000 kwa kila goli litakalofungwa na timu ya Bomani endapo watashinda mechi hiyo.
Hatua hiyo imelenga kuinua morali ya vijana na kuhimiza ushindani wa kweli kwenye mashindano ya soka ngazi ya jamii. Hii ni sehemu ya mpango mpana wa kampuni hiyo kuwekeza kwenye maendeleo ya kijamii kupitia michezo, kama njia ya kukuza vipaji na kujenga mshikamano.
Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan
"Tunaunga mkono kwa dhati juhudi za Mheshimiwa Rais katika kuibadilisha tasnia ya michezo kuwa chombo cha maendeleo ya kiuchumi na kijamii. Kama kampuni, tunawajibika kushiriki kikamilifu katika kuibua na kuinua vipaji vya vijana wetu," alisema Mheshimiwa Chacha Soya.
Timu ya Bomani FC imepokea motisha hiyo kwa hamasa kubwa, huku mashabiki wakijitokeza kwa wingi kuipa sapoti timu yao. Wadau wa michezo wamepongeza juhudi za SOYA ONE LIMITED wakisema kuwa mfano huu unapaswa kuigwa na kampuni nyingine nchini.
Kwa muda mrefu sasa, SOYA ONE LIMITED imejijengea heshima kama mdau mkubwa wa maendeleo katika mkoa wa Mara, ikiwa mstari wa mbele kusaidia sekta mbalimbali kama elimu, afya, mazingira na sasa michezo – yote yakiwa chini ya kauli mbiu yao: “Jamii Kwanza.”


Comments
Post a Comment