RAIS SAMIA ALETEA TARIME KITUO CHA POLISI CHA KISASA
Pichani ni Ujenzi Wa Kituo Cha polisi Cha Kisasa Tarime Mjini
Tarime, Mara – Wananchi wa Tarime mjini wanashuhudia maendeleo makubwa katika sekta ya usalama baada ya kuanza kwa ujenzi wa kituo cha polisi cha kisasa aina ya gorofa, mradi unaosimamiwa na serikali chini ya uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan.
Mradi huu, ambao upo katika hatua za awali za ujenzi, unatarajiwa kuimarisha huduma za ulinzi na usalama kwa wakazi wa Tarime na maeneo jirani. Picha zinazoonyesha mafundi wakiendelea na kazi, vifaa vya ujenzi vikiwa vimeletwa kwa wingi, ni ishara kwamba serikali imedhamiria kuboresha miundombinu ya Jeshi la Polisi katika mkoa wa Mara.
Mmoja wa wananchi waliopo eneo la ujenzi ameeleza furaha yake kwa hatua hii, akisema: "Kwa muda mrefu tumekuwa na changamoto ya uhaba wa kituo cha kisasa cha polisi hapa mjini, lakini sasa tunaiona kazi ya Rais Samia ikitekelezwa kwa vitendo."
Kituo hicho kipya kitakuwa na ofisi za kisasa, vyumba vya mahojiano, na sehemu za kuhifadhi watuhumiwa kwa mujibu wa viwango vya kisasa vya Jeshi la Polisi. Hatua hii ni sehemu ya jitihada za serikali kuhakikisha usalama wa wananchi na kuboresha mazingira ya kazi kwa askari polisi.
Serikali imesisitiza kuwa ujenzi wa kituo hiki ni sehemu ya mpango mpana wa kuboresha miundombinu ya usalama katika mikoa mbalimbali nchini, huku ikiendelea kuwekeza katika maendeleo ya sekta nyingine muhimu kama elimu, afya, na barabara.
Wananchi wa Tarime wanahimizwa kushirikiana na vyombo vya usalama na kutoa usaidizi unaohitajika ili kuhakikisha mradi huu unakamilika kwa wakati na kwa viwango bora.
Imeandikwa na Daniel yohana mussa
WhatsApp; +255656114799


Comments
Post a Comment