Posts

MKUU WA WILAYA YA TARIME AKABIDHI MIZINGA KWA WAZEE WA KOO 12 WAZEE WAMSHUKURU NA KUTOA PONGEZI KWA SOYA ONE NA WADAU WENGINE

Image
  Tarime, Julai 28, 2025 Mkuu wa Wilaya ya Tarime, Meja Edward Gowele, ameendesha tukio maalum la kukabidhi mizinga ya nyuki kwa wazee wa koo zote kumi na mbili za Tarime Mjini na Vijijini, ikiwa ni hatua ya kuwaheshimu, kuwawezesha kiuchumi, na kutambua mchango wao mkubwa katika kulinda amani na utulivu wa jamii. Akizungumza katika hafla hiyo, Meja Gowele alisema kuwa wazee ni nguzo kuu ya hekima, mshikamano na maadili katika jamii, hivyo ni wajibu wa serikali na jamii kwa ujumla kuendelea kuwathamini na kuwawezesha ili waweze kushiriki kikamilifu kwenye maendeleo. “Leo tunawakabidhi mizinga hii ya nyuki si tu kama njia ya kuwawezesha kiuchumi, bali kama alama ya heshima na shukrani kwa nafasi yenu muhimu katika jamii. Mmetufundisha kuwa amani huanza nyumbani, na nyinyi mmekuwa walinzi wakuu wa hilo,” alisema Meja Gowele. Katika hatua ya kuonyesha mshikamano wa pamoja, Mkuu huyo wa Wilaya aliwashukuru kwa dhati wadau wote walioguswa na kutoa mchango wao kufanikisha zoezi hilo. Wad...

SOYA ONE LIMITED YAMUUNGA MKONO MHANDISI WA MADINI MKOA WA MARA, YAMPA PONGEZI KWA UTENDAJI WAKE BORA

Image
PICHANI NI MHANDISI MSUYA OFISI YA MADINI MKOA WA MARA Tarime, Juni 7, 2025 Kampuni ya Soya One Limited chini ya uongozi wa Mkurugenzi wake mahiri, Chacha Soya, imetoa pongezi za dhati kwa Mhandisi wa Madini Mkoa wa Mara, Mhandisi Amin Msuya, kwa kazi nzuri na ya mfano anayofanya katika kusimamia sekta ya madini mkoani humo. Kupitia taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa leo, Chacha Soya alisema kuwa kampuni yake, ambayo inajihusisha na shughuli za uchimbaji na usimamizi wa madini kwa kuzingatia misingi ya uwajibikaji kwa jamii, imeridhishwa na namna ambavyo ofisi ya Afisa Madini Mkazi wa Mkoa wa Mara inatekeleza majukumu yake kwa weledi, uwazi na kasi inayolenga maendeleo ya wachimbaji na ustawi wa uchumi wa mkoa. > "Kwa niaba ya Soya One Limited, napenda kumpongeza Mhandisi Amin Msuya kwa kazi nzuri anayoifanya. Ameonesha mfano wa uongozi bora kwa kushirikiana na wadau wote wa sekta ya madini bila ubaguzi, huku akihakikisha mazingira rafiki ya uwekezaji na uchimbaji yanaim...

SOYA ONE LIMITED YAIPONGEZA SERIKALI KWA KUWAWEZESHA WACHIMBAJI WADOGO NA KUIUNGA MKONO SEKTA YA MADINI

Image
PICHANI NI MKURUGENZI WA SOYA ONE LIMITED NDG CHACHA SOYA MUSOMA, JUNI 7, 2025 Kampuni ya Soya One Limited imetoa pongezi za dhati kwa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa hatua madhubuti inazochukua katika kuwawezesha na kuwashika mkono wachimbaji wadogo wadogo wa madini nchini, hususan katika mkoa wa Mara. Akizungumza mara baada ya kukamilika kwa kongamano kubwa la wachimbaji wa madini wa Mkoa wa Mara lililofanyika tarehe 6 Juni 2025 katika viwanja vya Mkendo, Musoma Mjini, Mkurugenzi wa Soya One Limited, Ndugu Chacha Soya, amesema kuwa mafanikio ya sekta ya madini yanaakisi juhudi za serikali ya awamu ya sita katika kuhakikisha wachimbaji wadogo wanapewa mazingira bora ya kufanya kazi kwa tija na usalama. "Natoa shukrani za dhati kwa Serikali kwa kuendelea kutambua mchango wa wachimbaji wadogo, lakini zaidi kwa hatua ya kuwajengea uwezo na kuwawekea mazingira rafiki ya kuchangia pato la taifa," alisema Ndugu Chacha Soya. "Sisi kama Soya One Limited, tunaion...

GWAJIMA AACHE KUCHEZEA AMANI YA TAIFA, NA MHE. RAIS SAMIA AANGALIE JICHO LA CHINI YA KIVULI HIKI

Image
PICHANI NI MWANAHABARI DANIEL MUSSA Na: Daniel Mussa Mwanahabari, Mtanzania Mzalendo, Tarime Kuna wakati wa kukaa kimya. Na kuna wakati wa kusimama na kusema kwa nguvu zote. Sasa ni ule wakati. Kwa siku kadhaa sasa, taifa letu limetikiswa na kauli za Askofu Josephat Gwajima Mbunge wa Kawe, ambaye badala ya kutenda kazi za uongozi na uwakilishi, amegeuza jukwaa lake kuwa kiwanda cha tuhuma, vitisho, na propaganda chafu. Amediriki kutumia jina la hayati Dkt. John Pombe Magufuli akijivika mavazi ya mashujaa, ilhali kwa ndani akipanda mbegu za uchochezi. Kauli yake ya “nileteeni Gwajima” ambayo aliwahi kusemewa na Magufuli, sasa anaitumia kama kibali cha kuasi nidhamu ya chama, kupinga serikali, na kudhoofisha jitihada za Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan katika kulijenga taifa la maridhiano, mageuzi ya kiuchumi, na diplomasia ya matumaini. Pichani ni Mheshimiwa Joseph Gwajima Hivi tunamwambiaje Rais Samia anayepambana kila siku kusafisha nchi na kuijenga upya, kuwa kuna watu wanaomchimba kisi...

SOYA ONE LIMITED YAKONGA NYOYO ZA WAUGUZI TARIME MJINI – YACHANGIA MAMILIONI KWENYE HARAMBEE YA UNUNUZI WA GARI LA WAFANYAKAZI WA AFYA

Image
  Pichani ni Mkurugenzi wa kampuni ya Soya One Limited  Na Daniel Mussa, Tarime Katika kuendeleza moyo wa uwajibikaji kwa jamii, kampuni ya SOYA ONE LIMITED, inayojishughulisha na uchimbaji wa madini na yenye makao yake katika Kata ya Kenyamanyori, wilayani Tarime, imetoa mchango mkubwa wa fedha katika harambee ya kuchangia ununuzi wa gari kwa ajili ya wafanyakazi wa afya wa Halmashauri ya Mji Tarime. Shughuli hiyo ilifanyika katika ukumbi wa BlueSky, ambapo ilihudhuriwa na mamia ya watumishi wa sekta ya afya, viongozi wa serikali, na wadau wa maendeleo. Mkurugenzi wa SOYA ONE LIMITED, Bw. Chacha Soya, alikuwa mgeni rasmi na alikabidhi mchango wa mamilioni ya shilingi kusaidia kutimiza azma ya ununuzi wa gari aina ya Coster, litakalosaidia katika usafiri wa pamoja wa wafanyakazi wa afya kwa shughuli mbalimbali. "Tumeguswa na dhamira ya watumishi wetu wa afya kutafuta suluhisho la changamoto zao kupitia harambee. Kama SOYA ONE LIMITED, hatukusita kushiriki kwa moyo mmoja kwa sa...

SOYA ONE LIMITED YAENDELEA KUNG’ARA KATIKA UDHAMINI WA ELIMU NA JAMII TARIME

Image
  Pichani Ni Mkurugenzi wa Soya One Limited ndg Chacha Soya akiwa na viongozi wa serikali Tarime, Mei 20, 2025 – Kampuni ya Soya One Limited inaendelea kudhihirisha dhamira yake ya dhati ya kusaidia jamii kupitia mchango wake mkubwa kwa shule na taasisi za kidini wilayani Tarime, ikiwa ni sehemu ya kaulimbiu yake ya “Jamii Kwanza.” Katika hatua hii kampuni hiyo imetoa gunia 10 za mahindi kwa shule za msingi Sabasaba, Mapinduzi na Azimio, kwa ajili ya chakula kwa wanafunzi. Pia, imeshughulikia gharama za kuunganishiwa umeme katika shule hizo tatu kwa kiasi cha Shilingi 836,577.52, hatua inayolenga kuboresha mazingira ya kujifunzia na kuongeza ufaulu. Kwa kuguswa na hali ya mwanafunzi mmoja mwenye changamoto ya kifedha, kampuni hiyo imetoa Shilingi 100,000 kumuwezesha kupata mahitaji muhimu ya shule na kuendelea na masomo bila vikwazo. Soya One Limited pia imeelekeza msaada wake kwa Shule ya Msingi Magufuli ya watoto wenye mahitaji maalum kwa kutoa gunia tano za mahindi, sukari na ho...

MANCHARE HECHE ATOA MCHANGO WA MILIONI MOJA NA MAJI KATONI 40 KATIKA KIKAO CHA HALMASHAURI KUU CCM TARIME

Image
PICHANI NI MJUMBE MKUTANO MKUU CCM TAIFA NDG MANCHARE HECHE Habari kamili Na Daniel Mussa Tarimee, Mei 19, 2025 Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa, Wakili Manchare Heche, ameendelea kuonesha moyo wa kizalendo na kujitoa kwa ajili ya chama kwa kuchangia kiasi cha shilingi milioni moja pamoja na katoni 40 za maji katika kikao cha Halmashauri Kuu ya CCM Wilaya ya Tarime kilichofanyika jana, Mei 18, 2025, mjini Tarime. Mchango huo umetolewa ikiwa ni sehemu ya kuunga mkono juhudi za chama katika kuimarisha shughuli zake za kisiasa na kiutendaji ndani ya Wilaya ya Tarime. Tukio hilo limepokelewa kwa furaha na pongezi kutoka kwa viongozi mbalimbali wa chama waliohudhuria kikao hicho, wakiongozwa na Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Tarime. Akizungumza na MBC MEDIA mara baada ya kukabidhi msaada huo, Wakili Manchare Heche alisema kuwa anafanya hayo yote kwa lengo la kulisapoti Chama Cha Mapinduzi (CCM) ili liendelee kuimarika na kuleta maendeleo kwa wananchi. Aidha, amepongeza...