SWALI LA MHE ESTHER MATIKO WIZARA YA MAJI.

 


Je, lini mradi wa kutoa maji ziwa Victoria wa  Rorya -Tarime utakamilika maana kasi ya utekelezaji ni ndogo sana.


Sambamba na swali la msingi Mhe Esther Matiko ameuliza maswali mawili ya nyongeza kama ifuatavyo..


1. Mhe Mwenyekiti majibu ya serikali hayana uhalisia kwa kutuaminisha wananchi wa Tarime - Rorya kwamba mradi huu utakamilika Julai 2025


Mradi huu ni wa miaka mitatu (3), sasa hivi tunapoongea imepita miaka miwili na nusu na fedha iliyotolewa ni 21.9 Billion nje ya 134 Billion za mradi ambayo ni 16% tu na utekelezaji wa mradi ni 13%


Nataka kujua Mkandarasi wa mradi aliwasilisha hati mbili za malipo za 1.9 billion na 2.4 billion zaidi ya miezi sita imeshapita, lakini mmetoa 1.9 billion na ndio maana amerudi site na hajarudi kikamilifu. Ni lini serikali itamaliza kulipa ile 2.4 billion ambayo Hati hii ameitoa zaidi ya miezi sita iliyopita..?


2. Kwa sababu serikali imejiapiza kumaliza huu mradi 2025 Julai kwa hizo 86% kwa maana ya Billioni 112 zilizobaki na kwa sababu mradi huu unaenda kusaidia takribani wananchi laki saba na thelasini, inatoa picha ni wananchi kiasi gani hawana maji safi na salama.


Nataka kupata uhakika wa serikali ni kwa jinsi gani wanaenda kutimiza ahadi hii kwa kutoa hizo Billioni 112 ndani ya miezi sita (6) ili mkandarasi akamilishe mradi huu.?


Tazama na kusikiliza Majibu ya Serikali yaliyotolewa na Naibu Waziri wa Wizara hiyo

Comments