SAID CHAMBIRI AWEKA WAZI SAFARI YAKE YA SIASA ,AWAOMBA WANANCHI KUKIWAAMINI VIONGOZI WA CCM NA KUKIPA CHAMA( CCM) USHINDI

 


Na Mwandishi Wetu 


Kada wa chama cha Mapinduzi CCM na Mdau wa Maendeleo Said Chambiri Ambaye Pia Ni Mkurugenzi wa Hotel ya HillsideHotel iliyopo Tarime Ameieleza MBC MEDIA Juu Ya Safari yake ya Siasa Ndani ya Chama Cha Mapinduzi 

Said Chambiri Ameeleza Pia Sababu Za yeye Kuwa karibu na Chama Cha Mapinduzi 


Mimi nimezaliwa hapa hapa tarime na nimesoma hapa tarime Elimu Yangu Ya Juu nimepata Inje ya Tarime Lakini Pia 

Nimewekeza Tarime ninayo hotel ya kisasa inaitwa HillsideHotel @hillside_hotel_and_safaritours Mimi Mimi 

Nimefanya siasa inje ya Tarime Nipata Bahati Ya kushiriki kwenye program za Chama Nyingi Ndani ya Tarime Na Inje ya Tarime 

Nimefanya kampeni Jimbo la babati mjini na kufanikiwa kurudishwa ndani ya ccm 

Pia nimefanya kampeni temeke 

Na katika uchaguzi pia nimeshiriki Chaguzi Nyingi Sana Pia ikumbukwe kuwa 


Mimi ni mwanachama wa ccm Kwa muda Mrefu nimejiunga kwenye jumuiya ya uvccm mwaka 2004

  Nimeshawishika kuendelea na shughuri za siasa kwenye mji wa tarime kwa sababu ndo sehemu ambayo naishi na 

 Sasa tunaende kwenye ushindani wa Vyama pinzani hivyo Sisi kwa Wanachama Tunapaswa kukipa Chama Chetu Nguvu  

Lakini Pia Mimi Niweke wazi kuwa kwa sasa mimi sio mtia nia Ndani Ya Chama Chetu Ni wajibu Wetu kama wanachama sehemu yoyote unayo kuwa unaruhusiwa kuendelea na Shughuri za kichama Kwa Sasa nipo Tarime Hivyo Kama Mwanachama ninatakiwa kushiriki kwenye Shughuri Za Kichama Kuhakikisha Chama Chetu Kinapata Ushindi wa Kishindo 

 


Mimi ninapo kuwa sehemu ninafanya kazi ya Chama kama Mwanachama Pia ikumbukwe kuwa mimi nimewekeza tarime sheria inanitaka kurudisha asilimia kadhaa kwenye jamii  

Mfano mimi ninapo alikwa sehemu kama mgeni natoa pale kama mdau Kingine watanzania wanapaswa kukijua ni kwamba 

Mimi ninapata faida nyingi na Serikali ya mama samia 


Kama Mwanachama wa Ccm Ninapaswa kuwa karibu na Jamii yangu ili kusaidia Shughuri Za Maendeleo na Kumsapoti Mhe mbunge wetu Michael Kembaki Kwa sababu 

Hatuwezi Kumuachia majukumu yote yeye kutoa msada kumsubiria mbunge afanye mambo yote Tunaweza kujikuta tunapoteza hivyo sisi kama wanachama inabidi tufanye mambo mengine kutimiza adhima ya chama chetu na tukisema tunamuachia mbunge kazi zote hato weza tunaweza kwenda kupoteza na kinapopoteza chama hajapoteza mbunge kimepoteza chama 

Tupo kwenye safari ya kukiimarisha chama chetu "Amesema Said Chambiri"

 Pia Saidi Chambiri Amewataka Wanachama na Wananchi Kujitokeza kwa wingi kushiriki kwenye Uchaguzi Wa Serikali za Mitaa Na kukiamini Chama cha Mapinduzi 

Comments