JACK KANGOYE LENGO KUU NI KUHAKIKISHA CCM INASHINDA KWA ASILIMIA KUBWA KATA ZOTE TUNAZITAKA

TAZAMA HAMOJIANO YOTE HAPA

Nimekuja kushirikiana na wenzangu uchaguzi serikali za Mitaa ili kusaidia chama chetu Cha ccm kuweza kuendelea kushika dolla niligombea 2020 ila sikufanikiwa ila uvumilivu umenifanya mpaka Leo nipo hapa na viongozi wameona nimekomaa kisiasa na ndio maana mpaka sasa nipo hapa kushirikiana na chama maana uchaguzi ni gharama ko nimekuja ili kuweza kuja kutoa sapoti ya aina yeyote itakayo tia nguvu na kwa bahati nzuri Ccm Ina watu wanaojielewa na tukishirikiana naimani tutaenda kukishindisha chama kwa asilimia kubwa maana lengo letu chama cha mapinduzi Tarime ni kushinda Kata zote na Mimi kama Mimi nimesha wezesha na ntazidi Kuwezesha mpaka sasa nimesha fikia mabalozi na kuweza kuwatia shime ili chama cha mapinduzi kishinde kwa asilimia kubwa lakini pia wenyeviti unajua wanawatu wanao wasaidia kampeni ila pia nimeweza kuwafikia na kufanya jambo la kuwashika mkono Mimi kama jack kangoye nimewafikia wenyeviti wote na mabalozi wote maana lengo letu sio kuchanga tu ila pia ni kuwafikia mpaka wale wa chini wote.


Kuhusu vijana nataka niwashauri viongozi wenzangu vijana wakipiga Simu wapo bar tusiwanunulie pombe ila tufanye jambo kwa Vijana ili kesho yake asiwe tegemezi Tena Tarime Kuna frusa nyingi sana ukweli usemwe tu viongozi tumekuwa wa kwanza kudidimiza uchumi Tarime natamani sana kufanya jambo Tarime na kuzalisha ajira kwa Vijana na ndio maana nimekuja na ukiangalia nimekua mtu wa Kusapoti sana Vijana kwenye vitu na mwisho vijana wanagawana na kutokuendelea kwakua vijana wamekuwa wakitumiwa vibaya kwa kuweza kununuliwa na mtu akisha kununua akipata anakuacha kwakua alikupa pesa ukampa Ushindi na ndio maana inatokea hivyo Kila mtu anakuja anagombea ana Marengo yake kama nilivyo sema hapo mwanzo Tarime Kuna frusa nyingi mfano nikianzisha kiwanda Tarime na nikaajiri vijana nitakuwa nimepunguza sehemu kubwa ya vijana wanao tegemea au wanaotumiea vibaya na hilo ndio lengo langu kubwa.

JE UNAHABARI NA UNATAKA KUSHEA NASI TUICHAPISHE HAPA PIGA SIMU +255656114499 AU EMAIL moonglobal255@gmail.com


Comments

Popular posts from this blog

GWAJIMA AACHE KUCHEZEA AMANI YA TAIFA, NA MHE. RAIS SAMIA AANGALIE JICHO LA CHINI YA KIVULI HIKI

MKURUGENZI WA SOYA ONE LIMITED AWASISITIZA WAUMINI WA EAGT RONSOTI TARIME MJINI KUILINDA AMANI; AFANIKISHA UPATIKANAJI WA MCHANGO WA MILIONI 12, ACHANGIA MILIONI 8 NA ASINDIKIZWA KWA MILIONI 5

SOYA ONE LIMITED YAENDELEA KUNG’ARA KATIKA UDHAMINI WA ELIMU NA JAMII TARIME