KONGAMANO LA KIMATAIFA LA KISWAHILI HAVANA LAKAMILIKA KWA MAFANIKIO MAKUBWA

Humphrey Polepole, Balozi na Mkuu wa Kituo Havana


Awali ya yote na kwa kipekee tunamshukuru Mungu wetu wa Mbinguni, ambaye kwa Neema na Rehema zake ametupa kibali kufanikisha tukio hili kubwa lenye tija, faida, manufaa na maslahi mapana kwa Afrika, Lugha ya Kiswahili na wote wenye mapenzi mema na kiswahili kutoka Tanzania na Nje ya Tanzania 🇹🇿 


Pili tunamshukuru sana Mheshimiwa Mama Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania 🇹🇿 kwa Maelekezo yake, kukubali na kuwezesha Kongamano la Kimataifa la Kiswahili lifanyike hapa Havana Nchini Cuba 


Tatu, shukrani nyingi ziende kwa Serikali ya Jamhuri ya Cuba 🇨🇺 kwa kuona umuhimu, kuwapendeza na kusaidia Kongamano hili tuliandae pamoja katika nchi yao nzuri na rafiki yetu wa kudumu Cuba. 


Nne, Sina maneno ya kutosha kwa washiriki wa Kongamano la Kimataifa la Kiswahili ambao wamesafiri umbali mrefu na kwa gharama kubwa kuja kushiriki nasi katika tukio hili la kihistoria na ambalo limeiandika kipekee nafasi ya Tanzania na Afrika katika ukanda huu wa Karibe, Amerika ya Kati na Amerika ya Kusini, Mungu wa Mbinguni ninayemuamini akawaongeze maradufu kwa upendo huu mkubwa kwa Lugha ya kiswahili na Uwekezaji huu mkubwa mlioufanya, kama Mungu aishivyo ukawe na tija maradufu.


Tano, shukrani ziwaendee Viongozi wetu na watendaji wa Wizara yetu ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki kipekee Mhe. Waziri Balozi Mahmoud Thabit Kombo Jecha (Mb), Wizara ya Utamaduni Tanzania Mhe. Waziri Dkt. Damas Daniel Ndumbaro na Wizara ya Utamaduni Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Mhe. Waziri Tabia Mwita na Taasisi zao katika SMT na SMZ


Sita, kipekee asanteni sana Chuo Kikuu cha Dar Es Salaam (CKD) na Chuo Kikuu cha Havana (UH) kwa kuheshimisha Nchi zetu na kutoka na Kamusi ya Kwanza ya Lugha ya Kihispaniola na Kiswahili, huu ni mradi wa kimkakati na wenye tija kwa Nchi zetu mbili, sasa tunakwenda hatua ya pili


Saba, napenda kusema kwenye kila kazi nzuri anayofanya Kiongozi, nyuma yake wako watumishi wa umma hodari, madhubuti, wenye mbinu na maarifa anuai, weledi, waadilifu, wanaompenda, kumheshimu, kumwongoza na kumshauri vema Kiongozi wao. Mkiona nafanya vizuri mjue ilimpendeza Mamlaka nipewe wasaidizi hawa, na kama kuna pahala mkiona nimeteleza, mnisamehe, ni mimi mwenyewe na mapambano yangu ya kwenda kinyume na jina langu (Polepole). Asante sana na Mungu awabariki Wilbroad, Neema, Edward na watumishi wenzetu wote wenyeji wakiongozwa na Yanet. 

                  Daima #kataawahuni

Comments