BINTI CCM TARIME WAGAWA TAULO ZA KIKE
Pichani ni Ndugu Janeth Mtiba akiwa na wanafunzi wa shule za sekondari.
Ziara ya Binti Ccm Tarime ikiongonzwa na Kiongozi wa Binti Ccm Ndugu Janeth Mtiba imeweza kufika katika ukumbi wa shule ya sekondari Tarime ambapo wamekutana na wanafunzi wa shule za sekondari Iganana,Bomani ambapo wamegawa Taulo za kike Zenye Thamani Ya Tsh 2050,000/= (Million Mbili na Nusu) na Tarime sekondari Ambapo Mgeni Rasimi Ni Mbunge Viti Maalum mkoa wa Mara Ghati Chomete.
Pichani ni Mheshimiwa Mb Ghati ChometeAmezungumza na Wanafunzi Hao na kuwaasa Waweze kusoma kwa Bidii na kukataa Vishawishi vitakavyo sababisha kutofikia ndoto zao za kimasomo ambapo ameongea na kutoa Elimu Juu ya Ukatili wa kijinsia na Elimu juu ya hedhi salama lakini pia Ametoa zawadi kwa shule hizo kwa kuwapatia Viroba Vya Mchele Kg 50 kwa Kila shule ambapo jumla ni Kg 150 kwa Shule 3 pia ameweza kutoa mipira ya
ya mchezo wa miguu katika shule ya Tarime sekondari na kuhaaidi kuwapa zawadi zaidi kama wakifanya Vizuri zaidi na kuongeza divisheni one katika mitihani Ya Kitaifa
Walimu wa shule hizo wameweza kumshukuru Mheshimiwa Ghati Chomete mbunge Viti maalum sambamba na Janeth Mtiba Ambae ni Kiongozi wa Binti Ccm Tarime na kumpongezaGhati Chomete kwa juhudi zake za kimaendeleo Katika Mkoa wa Mara hususa ni Katika shule hizo na zingine zote alizoweza kuzitembelea na kuwashika Mkono pale Wanapo mwitaji.
Comments
Post a Comment