CHONCHORIO ACHANGIA MILION MOJA UJENZI WA KANISA LA WAADVENTISTA WASABATO NYAMITEMBE
Pichani juu ni Mjumbe wa Mkutano Mkuu Wa Ccm Taifa (Ndg Daniel Chonchorio )
Na Daniel Yohana Musa, Tarime Mjini
Mjumbe wa Mkutano Mkuu Wa Ccm Taifa, Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Ccm Mkoa Wa Mara Ndg Daniel Chonchorio ametoa Sh milioni 1 kuchangia ujenzi wa Kanisa la Waadventista Wasabato Nyamitembe
Iliyopo Kata ya Nkende Tarime Mjini.
(Pichani ni Mzee Champsi)Ndg Champsi pamoja na kuwasilisha mchango huo kwa niaba ya Mjumbe wa Mkutano Mkuu Wa Ccm Taifa Ndg Daniel Chonchorio ameongoza Changizo .
Akizungumza Kwa Njia Ya simu baada ya harambee hiyo ameahidi Mjumbe wa Mkutano Mkuu Wa Ccm Taifa Ndg Daniel Chonchorio ataendelea kutoa ushirikiano katika shughuli za maendeleo ya Kanisa hilo na kuomba liendelee kuliombea Taifa letu amani
Pia ameshukuru Viongozi wa Dini kuendelea Kuliombea Taifa Haswa Wakati Huu wa Uchanguzi Wa Serikali Za Mitaa Na kuwaomba Kujitokeza Kushiriki Uchaguzi Huo.


Comments
Post a Comment