SOYA ONE LIMITED YAENDELEA KUNG’ARA KATIKA UDHAMINI WA ELIMU NA JAMII TARIME
Pichani Ni Mkurugenzi wa Soya One Limited ndg Chacha Soya akiwa na viongozi wa serikali Tarime, Mei 20, 2025 – Kampuni ya Soya One Limited inaendelea kudhihirisha dhamira yake ya dhati ya kusaidia jamii kupitia mchango wake mkubwa kwa shule na taasisi za kidini wilayani Tarime, ikiwa ni sehemu ya kaulimbiu yake ya “Jamii Kwanza.” Katika hatua hii kampuni hiyo imetoa gunia 10 za mahindi kwa shule za msingi Sabasaba, Mapinduzi na Azimio, kwa ajili ya chakula kwa wanafunzi. Pia, imeshughulikia gharama za kuunganishiwa umeme katika shule hizo tatu kwa kiasi cha Shilingi 836,577.52, hatua inayolenga kuboresha mazingira ya kujifunzia na kuongeza ufaulu. Kwa kuguswa na hali ya mwanafunzi mmoja mwenye changamoto ya kifedha, kampuni hiyo imetoa Shilingi 100,000 kumuwezesha kupata mahitaji muhimu ya shule na kuendelea na masomo bila vikwazo. Soya One Limited pia imeelekeza msaada wake kwa Shule ya Msingi Magufuli ya watoto wenye mahitaji maalum kwa kutoa gunia tano za mahindi, sukari na ho...