OROMBE CUP YAMALIZIKA SUSUNI ,WAISHUKURU SOYA ONE LIMITED KWA KUWA CHACHU YA MAENDELEO KWENYE JAMII

 




Na Ernest Makanya 


mashindano ya Orombe Cup yaliyokuwa yakifanyika katika uwanja wa Shule ya msingi Susuni 


mashindano hayo yamemalizika Jana Agositi 28,2022 ambapo mshindi wa kwanza alipata zawadi ya shilingi  Laki tatu huku mshindi wa pili. alipata laki mbili 


Akizungumza wakati wa kukabidhi zawadi hizo Afisa Tarafa Ndg Gradnes mtandu kwa Niaba ya Mkuu wa Wilaya Ya tarime Meja Edward Gowere amepongeza Wananchi Kujitokeza kwa wingi kwenye Fainal za michuano hiyo alisema mashindano hayo yamekuwa chachu katika Tarafa Ya Ichungu kwa kuhamasisha vijana kuto Jihusisha na mambo yanaweza kuharibu amani 



Gradnes ametoa wito kwa wakazi wa Wilaya Tarime kuwa wazalendo Pia Kujitokeza kwa Wingi Kushiriki Uchaguzi wa Serikali za Mitaa.


Akizungumzia Mafanikio ya Michuano hiyo Diwani Viti MaalumTarafayaIchungu Mhe Josephine  Orombe,amesema kuwa Alishawishika zaidi Kuwekeza kwenye michezo kwani michezo inawaleta watu pamoja hata hivyo Mhe Orombe Ameishukuru Soya One Limited kwa kuendelea kuwa karibu na jamaii amesema alivyo mfikia Mkurugenzi wa Soya One Limited Kuomba kudhamini michuano hiyo wala hakusita kufanya hivyo nipende kutoa shukuran zangu za dhati kwa soya One Limited kwa njinsi ambavyo wemekuwa karibu na jamii niwapongeze sana 


Mhe Orombe Ambaye alikuwa mdhamini mkuu wa mashindano hayo kwa kushirikiana na Soya One Limited alisema mashindano hayo waliyaanzisha kwa lengo la kuhamasisha jamii kuwekeza kwa michezo pia Kushiriki Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 


Naye Katibu Wa Uwt Kata ya Susuni alisema mashindano hayo yamefikia malengo kwa asilimia 90 huku akimuomba Mhe Diwani kuwekeza pia kwa jinsia ya ke pia na wao wanatamani kushiriki kwenye michezo 

 

Naye Mc Mnyama amesema Mashindano haya yamekuwa ya aina yake tumekuwa na mashirikiano mbalimbali lakini haya yamekuwa ya tofauti hata hivyo nimuombe mhe diwani kwa kipindi kingine asisite kufanya hivi maana michezo inawaepusha vijana na mambo mengi ikiwemo vikundi vibaya ,kujihusisha na utumiaji wa madawa ya kulevya ,vitendo vya kiuharifu sasa wanakuwa kwenye michezo 

Pia niwashukuru soya One Limited kwa kumshika mhe Diwani kwenye michezo hii wameweza kuongeza mvuto zaidi kwenye michezo hii .










Comments

Popular posts from this blog

GWAJIMA AACHE KUCHEZEA AMANI YA TAIFA, NA MHE. RAIS SAMIA AANGALIE JICHO LA CHINI YA KIVULI HIKI

MKURUGENZI WA SOYA ONE LIMITED AWASISITIZA WAUMINI WA EAGT RONSOTI TARIME MJINI KUILINDA AMANI; AFANIKISHA UPATIKANAJI WA MCHANGO WA MILIONI 12, ACHANGIA MILIONI 8 NA ASINDIKIZWA KWA MILIONI 5

SOYA ONE LIMITED YAENDELEA KUNG’ARA KATIKA UDHAMINI WA ELIMU NA JAMII TARIME