CHONCHORIO ALIVYO ONGEZA MVUTO ZOEZI LA UCHUKUAJI WA FOMU ZA KUGOMBEA SERIKALI ZA MITAA JIMBO LA TARIME MJINI
Na Ernest makanya, Tarime Mjini
Maandamano yaliyo anzia Ofisi Za Chama Cha Mapinduzi Wilaya Ya Tarime Kuelekea Kwenye Vituo Vya kuchukuria Fomu Za Kugombea Serikali Za Mitaa Yameongozwa na Mjumbe Wa Mkutano Mkuu Wa Ccm Taifa Ndg Daniel Chonchorio ambapo wagombea nafasi za uenyeviti wa mitaa Jimbo la Tarime Mjini wakienda kuchukua fomu ofisi ya msimamizi wa uchaguzi wa serikali
Baadhi ya wagombea nafasi ya uenyeviti wa mitaa kupitia Chama cha Mapinduzi CCM Wameongozana na Mjumbe wa Mkutano Mkuu Wa Ccm Taifa Ndg Daniel Chonchorio Wamepita kila kituo Kuhakikisha zoezi Linakwenda vizuri
Wagombea saba nafasi ya Mwenyekiti wa serikali za mitaa kupitia Ccm Wilaya Ya Tarime wamechukua fomu za serikali za kugombea nafasi hiyo katika uchaguzi ujao wa serikali za mitaa Novemba 27 mwaka huu.
Zoezi hilo limefanyika Leo Oktoba 28,2024 likiambatana na maandamano ya kutembea kwa miguu kuanzia Ofisi Za Chama Cha Mapinduzi Wilaya Ya tarime kuelekea ofisi ya msimamizi wa uchaguzi kisha kumalizikia katika viwanja vya ofisi ya Ccm Wilaya
Akizungumza baada ya uchukuaji fomu hizo Mjumbe wa Mkutano Mkuu Wa Ccm Taifa Ndg Daniel Chonchorio amewataka wagombea na wanaCCM wote kuendelea kuwa watulivu wakingojea muda wa kampeni huku wakiendelea kuonesha umoja kama walivyoonesha kwa kuwasindikiza.
Ndg zangu haya yote tunayo yafanya tunaunga juhudi za chama chetu cha Mapinduzi ccm Chini ya mwenyekiti ccm taifa Dkt Samia Suruhu Hasani tunaona kazi kubwa imefanyika hivyo tunavyo vya kuwambia wananchi wetu Tuendeshe zoezi hili kwa amani na utulivu "Amesema Chonchorio "
Kwa upande wake Mjumbe Wa Halmashauri Kuu ya Ccm Mkoa Wa Mara Ndg Godfrey Gariba amewapongeza wagombea wote walioshiriki kugombea ndani ya Chama na kisha kupatikana baadhi watakaopeperusha bendera ya Chama hicho kuwa hayo yote ni maamuzi ya wanachama wenyewe wanachotakiwa kufanya ni kushirikiana,kuungana,kupendana




Comments
Post a Comment