GWAJIMA AACHE KUCHEZEA AMANI YA TAIFA, NA MHE. RAIS SAMIA AANGALIE JICHO LA CHINI YA KIVULI HIKI
PICHANI NI MWANAHABARI DANIEL MUSSA Na: Daniel Mussa Mwanahabari, Mtanzania Mzalendo, Tarime Kuna wakati wa kukaa kimya. Na kuna wakati wa kusimama na kusema kwa nguvu zote. Sasa ni ule wakati. Kwa siku kadhaa sasa, taifa letu limetikiswa na kauli za Askofu Josephat Gwajima Mbunge wa Kawe, ambaye badala ya kutenda kazi za uongozi na uwakilishi, amegeuza jukwaa lake kuwa kiwanda cha tuhuma, vitisho, na propaganda chafu. Amediriki kutumia jina la hayati Dkt. John Pombe Magufuli akijivika mavazi ya mashujaa, ilhali kwa ndani akipanda mbegu za uchochezi. Kauli yake ya “nileteeni Gwajima” ambayo aliwahi kusemewa na Magufuli, sasa anaitumia kama kibali cha kuasi nidhamu ya chama, kupinga serikali, na kudhoofisha jitihada za Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan katika kulijenga taifa la maridhiano, mageuzi ya kiuchumi, na diplomasia ya matumaini. Pichani ni Mheshimiwa Joseph Gwajima Hivi tunamwambiaje Rais Samia anayepambana kila siku kusafisha nchi na kuijenga upya, kuwa kuna watu wanaomchimba kisi...

















Comments
Post a Comment