PICHANI NI MWANAHABARI DANIEL MUSSA Na: Daniel Mussa Mwanahabari, Mtanzania Mzalendo, Tarime Kuna wakati wa kukaa kimya. Na kuna wakati wa kusimama na kusema kwa nguvu zote. Sasa ni ule wakati. Kwa siku kadhaa sasa, taifa letu limetikiswa na kauli za Askofu Josephat Gwajima Mbunge wa Kawe, ambaye badala ya kutenda kazi za uongozi na uwakilishi, amegeuza jukwaa lake kuwa kiwanda cha tuhuma, vitisho, na propaganda chafu. Amediriki kutumia jina la hayati Dkt. John Pombe Magufuli akijivika mavazi ya mashujaa, ilhali kwa ndani akipanda mbegu za uchochezi. Kauli yake ya “nileteeni Gwajima” ambayo aliwahi kusemewa na Magufuli, sasa anaitumia kama kibali cha kuasi nidhamu ya chama, kupinga serikali, na kudhoofisha jitihada za Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan katika kulijenga taifa la maridhiano, mageuzi ya kiuchumi, na diplomasia ya matumaini. Pichani ni Mheshimiwa Joseph Gwajima Hivi tunamwambiaje Rais Samia anayepambana kila siku kusafisha nchi na kuijenga upya, kuwa kuna watu wanaomchimba kisi...
MKURUGENZI WA SOYA ONE LIMITED (CHACHA GESORA) Tarime Mjini, Tanzania – Mkurugenzi wa Soya One Limited, Chacha Soya, ameendelea kuonyesha moyo wa kujitoa kwa jamii baada ya kufanikisha upatikanaji wa mchango wa jumla ya shilingi milioni 12, ambapo mwenyewe alichangia milioni 8, na waumini pamoja na wageni wengine wakasindikiza kwa milioni 5. Mkurugenzi huyo alialikwa rasmi kama mgeni maalum katika ibada ya Jumapili iliyofanyika katika Kanisa la EAGT Ronsoti, ibada iliyojaa uwepo wa Mungu na iliyoongozwa na Mchungaji Maswi. Katika hotuba yake yenye kugusa mioyo, Mkurugenzi Soya alisisitiza umuhimu wa kulinda amani ya nchi akisema: “Amani yetu ni nguzo ya maendeleo. Tanzania imebarikiwa na Mungu kwa utulivu wake. Tuilinde, tuiombee, na tuishi kama watu wanaothamini urithi huu adhimu.” Alisisitiza kuwa amani ndiyo msingi wa ibada, biashara, uchumi na ustawi wa familia, hivyo kila Mwanatarime na Mtanzania kwa ujumla ana wajibu wa kuwa mlinzi wa amani. Katika kuendelea kusapoti k...
Pichani Ni Mkurugenzi wa Soya One Limited ndg Chacha Soya akiwa na viongozi wa serikali Tarime, Mei 20, 2025 – Kampuni ya Soya One Limited inaendelea kudhihirisha dhamira yake ya dhati ya kusaidia jamii kupitia mchango wake mkubwa kwa shule na taasisi za kidini wilayani Tarime, ikiwa ni sehemu ya kaulimbiu yake ya “Jamii Kwanza.” Katika hatua hii kampuni hiyo imetoa gunia 10 za mahindi kwa shule za msingi Sabasaba, Mapinduzi na Azimio, kwa ajili ya chakula kwa wanafunzi. Pia, imeshughulikia gharama za kuunganishiwa umeme katika shule hizo tatu kwa kiasi cha Shilingi 836,577.52, hatua inayolenga kuboresha mazingira ya kujifunzia na kuongeza ufaulu. Kwa kuguswa na hali ya mwanafunzi mmoja mwenye changamoto ya kifedha, kampuni hiyo imetoa Shilingi 100,000 kumuwezesha kupata mahitaji muhimu ya shule na kuendelea na masomo bila vikwazo. Soya One Limited pia imeelekeza msaada wake kwa Shule ya Msingi Magufuli ya watoto wenye mahitaji maalum kwa kutoa gunia tano za mahindi, sukari na ho...
Comments
Post a Comment